Mshauri wa Kimataifa wa Kujitegemea, James Rugemalira (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari wakati wa majumuisho ya ziara ya Profesa Pais ya kutembelea mikoa kadhaa nchini. Kutoka kulia ni Dk. Sima Rugarabamu wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Mkurugenzi wa Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits LTD, Benedicta Rugemalira na Profesa Pais.
Profesa Pais (kushoto), akitoa majumuisho ya ziara yake hiyo. Kulia Mkurugenzi wa Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits LTD, Benedicta Rugemalira, ambayo ilidhamini ziara hiyo. Mshauri wa Kimataifa wa Kujitegemea, James Rugemalira (kushoto) na Mkurugenzi wa Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits LTD, Benedicta Rugemalira (kulia), wakimpa zawadi Profesa Pais baada ya kutoa majumuisho hayo.
Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo.
Wadau wa sekta ya afya wakiwa kwenye mkutano huo uliofanyika Hoteli ya Protea Court Yard Seaview jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Joe Mgaya, Dk.Fred Limbanga, Mkurugenzi wa Mabibo, Benedicta Rugemalira na .Dk. Sima Rugarabamu wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Wadau wa sekta ya afya pamoja na maofisa wa Kampuni ya Mabibo wakiwa kwenye mkutano huo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Usalama na Maghara wa Mabibo Beer, Boniface.
Mshauri wa Kimataifa wa Kujitegemea, James Rugemalira (kulia), akiwa kwenye mkutano huo. Kushoto ni Dk.Fred Limbanga na mmoja wa wakurugenzi, Respicius Didace.
Dk. Sima Rugarabamu wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (kulia), akisisitiza jambo katika mkutano huo.Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.
HATUA mahususi na za haraka zinahitajika kukabiliana na ugonjwa wa saratani ambao umegeuka kuwa tishio hapa nchini.
Hayo yalisemwa na daktari bingwa wa ugonjwa huo, hususani saratani ya matiti kutoka India, Profesa Anthony Pais, jana jijini Dar es Salaam katika majumuisho ya ziara yake aliyoifanya katika mikoa mbalimbali kuangalia ukubwa wa ugonjwa huo.
Akiwa ameongozana na viongozi wa kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Limited, iliyodhamini ziara hiyo, daktari huyo ameshauri kuwa kuna umuhimu wa kujenga kituo kikubwa cha kimataifa hapa nchini kitakachoshughulikia ugonjwa huo ili kupunguza gharama za kupeleka wagonjwa nje ya nchi.
Akiwa ameongozana na viongozi wa kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Limited, iliyodhamini ziara hiyo, daktari huyo ameshauri kuwa kuna umuhimu wa kujenga kituo kikubwa cha kimataifa hapa nchini kitakachoshughulikia ugonjwa huo ili kupunguza gharama za kupeleka wagonjwa nje ya nchi.
"Nimegundua kuna vituo viliwili, kimoja Ocean Road na Hospitali ya Muhimbili. Lakini tatizo la saratani kwa sasa Tanzania ni kubwa na linahitaji kushughulikiwa kwa haraka.
Ningependelea kuwepo na vituo viwili vikubwa. Kimoja Mwanza na kingine Bukoba ili kuhudumia hata nchi jirani," alisema.
Ameeleza kuwa katika ziara aliyoifanya katika mikoa ya Morogoro, Dodoma, Kagera na Mwanza, amegundua kuwa kuna aina kuu tatu za saratani ambazo zinasumbua wananchi wengi na kumekuwepo na msululu wa wagonjwa wakipelekwa India kupata matibabu kwa gharama kubwa.
Dk Pais amezitaja aina hizo za saratani kama saratani ya matiti, saratani ya kibofu cha mkojo na saratani ya shingo ya uzazi. Alieleza kuwa wagonjwa wengi wamekuwa wakigundulika kuwa na saratani hizi wakati tayari zimeshafikia hatua ya kutisha.
"Hivyo tukiwa na vituo hapa hapa Tanzania vya kupima na kutibu ugonjwa huu itasaidia wagonjwa kujulikana mapema na baadae kupata tiba haraka tena kwa bei nafuu. Mimi niko tayari kutoa mafunzo kwa wahusika mbalimbali kutoka madaktari hadi wahudumu. Kwa pamoja tunaweza," alisema.
Naye Mshauri wa kujitegemea wa kimataifa wa Mabibo, James Rugemalira, ambaye kampuni yake husambaza vinywaji aina ya Windhoek Larger na Windhoek Draught hapa nchini, amemshukuru daktari huyo kwa kukubali kuja na kwa ushauri wake ambao utasaidia sana katika kukabiliana na ugonjwa huo.
Ameeleza kuwa mara kampuni yake itakapopokea taarifa ya kitaalaam kutoka kwa daktari huyo, Mabibio itaaanzia mchakato utakaofanikisha ujenzi wa vituo vingine vya kushughulikia ugomjwa wa saratani ili kupambana na tatizo hili hapa nchini.