Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando (wa pili kulia), akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, kuhusu onyesho la muziki lililoandaliwa na kitengo cha huduma kwa wateja kupitia Mradi wa 'Tunakujali' kwa ajili ya kukusanya pesa za kuchangia shule ya watoto wenye mahitaji maalum ya Pongwe mkoani Tanga, litakalowashirikisha wanamuziki nyota, Mzee King Kikii (wa pili kushoto) na Banana Zorro (kushoto), litakalofanyika kesho Septemba 03, katika viwanja vya Airtel Makao Makuu. Kulia ni Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa Airtel, Adriana Liamba.
Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa Airtel, Adriana Liamba (wa pili kulia), akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, kuhusu onyesho la muziki lililoandaliwa na kitengo cha huduma kwa wateja kupitia Mradi wa 'Tunakujali' kwa ajili ya kukusanya pesa za kuchangia shule ya watoto wenye mahitaji maalum ya Pongwe mkoani Tanga, litakalowashirikisha wanamuziki nyota, Mzee King Kikii (wa pili kushoto) na Banana Zorro (kushoto), litakalofanyika kesho Septemba 03, katika viwanja vya Airtel Makao Makuu. Kulia ni Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando.
Mwanamuziki nguli nchini, King Kikii akifafanua jambo kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, kuhusu ushiriki wake katika onyesho la muziki lililoandaliwa na kitengo cha huduma kwa wateja kupitia Mradi wa 'Tunakujali' kwa ajili ya kukusanya pesa za kuchangia shule ya watoto wenye mahitaji maalum ya Pongwe mkoani Tanga, litakalofanyika kesho Septemba 03, katika viwanja vya Airtel Makao Makuu. Kulia ni Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando (wa pili kulia), ni Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa Airtel, Adriana Liamba na Mwanamuziki nyota, Banana Zorro.
Kampuni Airtel Tanzania leo imetangaza kuanzisha mpango wa huduma kwa jamii utakaowashirikisha wafanyakazi wake kujitolea na kushiriki katika kuchangia na kusaidia jamiii nchini.
Mpango unategemea kuanza wiki hii unashirikisha wafanyakazi kutoka katika vitengo mbalimbali utawawezesha wafanyakazi hawa kuandaa shughuli zitakazowawezesha kukusanya fedha kwaajili ya kusaidia shule mbalimbali ambazo zina mahitaji muhimu katika maeneo mbalimbali nchini.
Mradi huu umezindulia rasmi na Kitengo cha huduma kwa wateja ndio kitakuwa cha kwanza kushiriki ambapo wameandaa burdani ya musiki itakayowashirikisha magwiji mahiri wa muziki nchini King KKii and Banana Zoro inayotegeme kufanyika siku ya jumatano tarehe 3 septemba 2014 katika viwanja vya ofisi ya Airtel. Wafanyakazi wa Airtel na watu mbalimbali kutoka nje wamealikwa kushiriki na kiasi cha pesa kitakachopatikana kitaenda kuchangia shule ya watoto wenye mahitaji maalum Tanga.
Akiongea kuhusu mpango huu Meneja Uhusiano wa Airtel Bwana Jackson Mmbando alisema” katika kushiriki kutatua changamoto mbalimbali zinazozikumba jamii wafanyakazi wa Airtel wameona ni muhimu kuanzisha mpango huu maalumu wa kusaidia jamii. Airtel kupitia mpango wake wa huduma kwa jamii umeonelea ni vyema kutenga siku 14 mahususi kwa wafanyakazi kupata muda wa kusaidia jamii.
Hivyo tutakuwa na shughuli mbalimbali kuanzia sasa zitakazofanya na wafanyakazi katika kukusanya fedha na kisha kufatiwa na siku 14 za kutoa misaada wa jamii zinazotegemea kuanza rasmi mwakani mwezi wa tatu. Lengo letu ni kuhakikisha tunazifikia shule 10 na kuzisaidia kwa sasa na leo tunachukua nafasi hii kuwaalika wafanyakazi wetu na jamiii kutuunga mkono na kushirikiana nasi”.
“Baadhi ya shule zitakzofaidika na mpango huu ni pamoja na shule ya Msingi Pongwe Tanga itakayojengewa darasa, shule ya msingi ya kumbukumbu Dar es salaam itapatiwa msaada wa viti na meza kwa darasa la watoto wa masomo ya awali, shule ya sekondari Ndala watapewa vifaa vya ofisi kwa wafanyakazi , uhuru mchanganyiko watanunuliwa mashine ya Braile pamoja na vifaa vya kufundishai na shule ya msingi kimara watapatiwa tanki ya kuhifadhi maji.
Nia yetu ni kuhakikisha tunazifikia shule nyingi zaidi na jamii kwa ujumla “aliongeza Mmbando.Airtel Tanzania imekuwa mstari wa mbele katika kusaidia sekta ya elimu nchini mpaka sasa zaidi ya shule 1000 zimeweza kufaidika na vitabu kupitia mradi wa Shule yetu” wiki iliyopita
Airtel imetangaza zaidi ya shule 30 zitakazofaidika na misaada ya vitabu kwa mwaka huu wa 2014 na leo kupitia wafanyakazi wake Airtel inaendelea kuwafikia watu wengi zaida na jamii nzima kwa ujumla nchini.