Wananchi wa Mwanagati-Kitunda jijini Dar es Salaam na maeneo jirani wamelilalamikia shirika la TANESCO kwa kukatiwa umeme kwa siku tatu mfululizo,bila taarifa yoyote kutolewa kwa wakazi hao.''hatuna umeme kwa siku 3 mfululizo usiku na mchana mpaka sasa na hakuna taarifa zozote toka shirika la umeme Tanesco kuelezea hali hii inayoendelea mpaka sasa'',alilalama mmoja wa wakazi wa eneo hilo.
Wakielezea kwa masikitiko makubwa juu ya tatizo hilo,Wananchi hao wamesema kuwa hawakupata taarifa yoyote ile toka Tanesco, na mpaka sasa wengi wao wamepata hasara kubwa kibiashara kutokana na tatizo hilo la kukosekana kwa umeme.
Mbali na matatizo hayo, Mji huo mpya ambao una chanzo chao cha kipekee kikubwa cha maji,kinachotegemea umeme katika uzalishaji wa maji na kufanya wananchi hao kukosa maji pia kwa siku 3 mfululizo na kufanya maisha yao kuwa magumu zaidi.
Tunaliomba shirika la TANESCO lisikilize kilio chetu haraka iwezekanavyo,na kuhakikisha tatizo la umeme linatatuliwa kwa wakati ili kutuepusha na adha tunayoipata sisi wakazi wa Managati-Kitunda
Juhudi za kuweza kuwapata wahusika toka shirika la umeme Tanesco ili kuelezea tatizo ili kwa wananchi wa Mwanagati - Kitunda zilishindikana mpaka tunapotoa habari hii.