Mwenyekiti wa Shirika la Afya na Elimu la Mikocheni, Bibi Kokushubila Kairuki akisoma hotuba katika maadhimisho ya miaka 14 ya Kumbukumbu ya siku ya Muasisi wa Shirika Hayati Prof. Hubert Kairuki. Alisema kuwa Tangu Muasisi huyo amefariki Februari 6, 1999, shirika lao limejiwekea utaratibu wa kumuenzi kwa kutenda yale mambo muhimu aliyokuwa akiyathamini wakati wa uhai wake.
Hayati Prof. Hubert Kairuki alithamini jitihada za serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali ya kuongeza idadi ya rasilimali watu kwenye fani za udaktari na uuguzi katika sekta ya afya. Ni katika jitihada hizo ndiyo aliamua kutoa mchango wake kwa kuanzisha shule ya Wauguzi ya Mikocheni (Mikocheni School of Nursing) na baadae kuanzisha Chuo Kikuu cha Tiba.
Aliongeza katika maadhimisho ya kumuenzi mwasisi huyo, shirika lao kwa mwaka 2013 wameamua kijikita katika mambo matatu; Kutoa elimu ya Afya kwa wanafunzi wa shule ya msingi Mikocheni. Pili, kutoa zawadi ya madawati yapatao 50 kwa shule hiyo ya msingi Mikocheni yenye thamani ya shilingi milioni 4,500,000/=. Tatu, Shirika kupitia chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki limetayarisha mhadhara kwa jamii 'Public Lecture' ambayo itatolewa na mwananzuoni Mtaalam Bingwa katika Afya ya jamii Prof. Theonesta Mutabingwa ambapo umelenga kutoa somo la matibabu ya ugonjwa wa malaria kwa wanawake wajawazito.
Wanafunzi wa shule ya msingi Mikocheni wakiimba wimbo kuwakaribisha wageni.
Mwenyekiti wa Shirika la Afya na Elimu la Mikocheni, Bibi Kokushubila Kairuki (kushoto) akifanya mahojiano na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza kutoa hotuba yake.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni na Diwani wa Kata ya Mikocheni, Yusuph Mwenda akiongea machache katika halfa hiyo. Pembeni yake ni Mwenyekiti wa Shirika la Afya na Elimu la Mikocheni, Bibi Kokushubila Kairuki.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana akitoa shukrani zake.
Wanahabari nao hawakuwa nyuma kunasa tukio.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana akipokea zawadi ya madawati kutoka kwa Mwenyekiti wa Shirika la Afya na Elimu la Mikocheni, Bibi Kokushubila Kairuk.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni na Diwani wa Kata ya Mikocheni, Yusuph Mwenda akitoa shukrani kwa Mwenyekiti wa Shirika la Afya na Elimu la Mikocheni, Bibi Kokushubila Kairuki mara baada ya kukabidhi zawadi hizo za madawati.
Wanafunzi wakifurahia mara baada ya kukabidhiwa kwa madawati hayo.
Mwenyekiti wa Shirika la Afya na Elimu la Mikocheni, Bibi Kokushubila Kairukia akiwa pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugombana (kushoto) na