Mwili wa Fredrick Mgaya (60) ukiwa unaning'inia katika mtu aliojinyongea, Tunaomba radhi kwa picha hii.
--------------------------
Habari kwa hisani ya Demashonews.
Mwanaume mmoja Fredrick Mgaya (60), mkazi wa Peramiho, Songea mkoani Ruvuma amejinyonga usiku wa kuamkia leo katika maeneo yaliyo karibu na viwanja vya michezo vya Abasia kijijini Peramiho.
Mwanaume huyo aliyekuwa akifanya kazi kitengo cha maabara katika Hospitali ya Peramiho na kustaafu mnamo mwezi aprili mwaka huu amekutwa amejinyonga majira ya asubuhi ya leo.
Marehemu Fredrick Mgaya amekutwa na ujumbe katika mfuko wa shati lake, ulioelezea chanzo kilichopelekea yeye kujitoa uhai.
Afande Allen Urio ambaye alikuwa mmoja wa mashuhuda wa kwanza,anasema “ Nilikuwa natoka lindo asubuhi ndipo nikakuta kundi la wanafunzi wa shule ya msingi wakiwa njiani, nikawauliza kwanini wamesimama badala ya kwenda shule muda ule, ndipo waliponiambia kuna mtu ananing’inia kwenye mti pale. Nilipofika kwenye mti huu ndipo nilipomkuta mzee
wetu Fredrick Mgaya akiwa ameshapoteza maisha.
Ni tukio la kusikitisha sana kwani ni mzee wetu katika jamii ambaye tulikuwa tunaishi naye vizuri. Mbali na migogoro yake na mkewe lakini uamuzi aliouchukuwa unasikitisha na si mzuri kabisa. Kama mlinda amani katika jamii napenda kuwaasa wananchi wajaribu kutafuta suluhu ya matatizo kwa namna nyingine na sio kwa kujitoa uhai”
Akiongea Hakimu wa mahakama ya mwanzo kijijini Peramiho bi Maria Sambo amesema, ameshaletewa na kusuluhisha migogoro ya ndoa hiyo ya marehemu mara mbili na hadi sasa kuna kesi inayoendelea katika mahakama ya Hakimu mkazi, lakini kwa hali ya kawaida hakudhani kwamba marehemu Fredrick Mgaya angefikia hatua hiyo ya kujitoa uhai.
Nao mashuhuda wa tukio hilo wakiongea kwa masikitiko, wengi wamelaani uamuzi uliofikiwa na mzee Mgaya kwani ni dhahiri alikuwa ni mtu wa watu na pia alikuwa ni tegemeo la familia yake ambayo amewaacha ghafla. Uamuzi ambao umesababisha maumivu kwa wanajamii hususan ndugu, jamaa pamoja na marafiki wengi waliokuwa wakimpenda na kushirikiana naye kwa mambo mengi ya kimaisha.
Mwenyekiti wa kijiji cha Peramiho A Bwana Joseph Ngonyani ameonesha masikitiko yake ya dhati kwa kuondokewa na
moja ya wazee aliokuwa akiwategemea kwa ushauri katika kijiji chake. “Tukio
hili linagusa sana unajua, kwasababu linahusu mtu wa karibu sana na ambaye
tunashinda nae siku zote bila kujua nini kinamsibu na nini anakipanga katika akili
yake”.
Ndoa nyingi sana zinasumbuliwa na migogoro ya hapa na pale, hivyo ni vizuri watu wa ustawi wa jamii na asasi zinazohusiana na jamii kujaribu kutoa mafunzo na maelekezo ya jinsi ya kutatua migogoro hiyo ili kuepusha adha kama hii isijitokeze tena ndani ya jamii yetu. Alisema mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo bwana Ignasi Kapinga.
Winfried Thadei Mgaya, mdogo wa marehemu
anasema, amepokea tukio hilo kwa mshtuko na kwa majonzi sana. Anapata uchungu
sana juu ya msiba wa kaka yake kwani marehemu ameacha watoto wanne ambao bado
ni tegemezi pamoja na mjane. Pia amesema mazishi yatafanyika tarehe 7
jumamosi kijijini kwao Madaba, Songea
mkoani Ruvuma,