Baadhi ya miili ya marehemu.
Watu zaidi ya 17 wanadaiwa kufariki dunia na wengine zaidi ya 50 kujeruhiwa baada ya mabasi waliokuwa wakisafiria kugongana katka k ijiji cha Mlogolo wilayani Sikonge mkoani Tabora.
Ajali hiyo imetokea leo hii jioni majira ya saa 11 jioni baada ya Basi la Kampuni ya Sabena lenye namba za usajiri T 110 ARV lililokuwa likitokea Mbeya kwenda Mwanza kumegongana uso kwa uso na basi la AM Dreamline lenye namba za usajiri T 803 ATN lililokuwa likitokea Mwanza kupitia Mpanda.
Ajali hiyo imetokea maeneo ya Mlogolo takribani kilometa 3 kutoka wilayani Sikonge.
Pia inadaiwa kuwa dereva wa basi la Sabena aliyefahamika kwa jina la James Kombe amepoteza maisha baada ya kukatika kiwiliwili na kufa papohapo a kuwa jitihada za kutafuta kiwiliwili chake zilikuwa zikifanyika baada ya kupondeka vibaya.
Mashuhuda wa ajali hiyo wamedai kuwa chanzo cha ajali hiyo ni madereva hao kuwa ni wasaidizi( Day-worker)
Inakadiriwa kuwa karibu robo tatu ya basi la sabena imeharibiwa vibaya sana.
Mabasi yaliyohusisha ajali hiyo ni basi la Sabena lililokuokea Mbeya kwenda -Mwanza na AM Dreamline lililokuokea Mwanza kwenda Mpanda.
Jitihada za kumpata Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP). Suzana Kaganda ili kuzungumzia ajali hiyo bado zinaendelea.