Quantcast
Channel: HABARI NA MATUKIO
Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

TUZO ZA WANAWAKE WENYE MAFANIKIO TANZANIA 2013 ZAZINDULIWA RASMI

$
0
0
Mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya Tanzania Women of Achievement (TWAA) Bi. Irene Kiwia (Kati) akiongea mbale ya waandishi wa habari wakati wa hafla ya uzinduzi wa Tuzo za Wanawake wenye Mafanikio Tanzania msimu wa 2013.
 ---
Taasisi ya Tanzania Women of Achievement (TWAA) leo imezindua Tuzo za Wanawake wenye Mafanikio Tanzania msimu wa 2013 zilizopangwa kufanyika katika siku ya wanawake duniani tarehe 8 Mwezi Machi mwaka huu.

Tuzo hizi ambazo hufanyika kila baada ya miaka miwili zilizinduliwa mwaka 2009 kwa heshima ya wanawake katika sekta mbalimbali nchini kote ambao kupitia kazi zao wamechangia kwa kiasi kikubwa sana kuleta maendeleo ya jamii zao kwa njia moja au nyingine.

"TWAA inataka kutambua wanawake, waishio Tanzania ambao kupitia kazi zao wameweza kupata mafanikio makubwa sit u kibinasi bali wametumia nafasi zao kuleta maendeleo na mabadiliko ya kimsingi kwenye jamii zinazowazunguka." Alisema Mkurugenzi mkuu wa TWAA Bi. Irene Kiwia. 

"Tuzo hizi mbazo sasa ziko katika msimu wake wa 3 zinatoa fursa nzuri ya kutambua na kupongeza wanawake ambao wamechangia sana kwenye kubadilisha na kuboresha sura ya Tanzania. Kwa wanawake wengi hii itakuwa mara ya kwanza mafanikio na michango yao imetunukiwa na hili ni jambo la kufajiri na kuridhisha sana.”

Vipengele vya tuzo za mwaka huu ni Sanaa na Utamaduni, Biashara na Ujasiriamali, Habari na Mawasiliano, Michezo, Professional (Kazi), Elimu, Afya, Ustawi wa Jamii, Sayansi na Teknolojia, Sekta ya Umma, Kilimo na Mshiriko Mdogo.

Bi Sadaka Gandi, mwenyekiti wa kamati ya TWAA alitoa wito kuwa "tunawasihi mashirika, vyama, wanawake na wanaume kote Tanzania kuteua wanawake wenye mafanikio katika makundi haya na kuonyesha mchango wao katika uwezeshaji wa wanawake. Kuna maelfu ya wanawake wastahili wa tuzo hizi huko nje ambao ni mawakala wa mabadiliko katika jamii zao. Tunataka kuimba mapambio ya mashujaa hawa na kuhamasisha mamilioni ya wanawake wengine wa Tanzania kuiga mifano na kupata msukumo wa kuleta mabadiliko. Kamati ilipokea fomu za nyingi sana za washiriki miaka ya nyuma na hivyo basi tunategemea ushiriki mzuri zaidi mwaka huu. "

Kamati ya TWAA inawajumuisha Bi Mary Rusimbi - Mwanaharakati na Mwanzilishi wa Programu ya Mtandao wa Jinsia Tanzania, Jaji Joaquine De Mello - Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Dk Marcelina Chijoriga- Mkurugenzi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Bi. Ludovicka Tarimo – Mtaalamu wa Jinsia kutoka USAID, Bwana. Innocent Mungy-Mkurugenzi wa Mawasiliano kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA), Sadaka Gandi - Mwanasaikolojia na mfanyakazi za Jamii, Irene Kiwia - Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya mahusiano ya jamii Frontline Porter Novelli.

Huko nyuma tuzo hizi zilidhaminiwa na Baileys, Delloite, NBC, Home Shopping Center, TCRA, Songas, Watu wa Marekani, DTP, UN DPG Gender Group, UNFPA, UNESCO, TBL, Multichoice, African Life Assurance, Barrick, Twiga Cement, Vodacom, Farm Equip, RBP, Clouds FM na Frontline Porter Novelli.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>