Quantcast
Channel: HABARI NA MATUKIO
Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

CASTLE LITE YAZINDUA PROMOSHENI KALI YA 'LITE UP THE WEEKEND'

$
0
0
Meneja masoko wa bia ya Castle lite Tanzania Vimal Vighmaria kushoto, Meneja wa kinywaji hicho Geofray Makau na meneja msaidizi wa Castle lite Victoria kimaro wakizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam kwenye uzinduzi wa kampeni ya kutafuta washindi wa kushiriki VIP YAchy Party ambapo kutakuwa na tamasha la burudani mbalimbali litakalofanyika katikati ya bahari ya hindi kwenye boat ya kisasa mwezi ujao.

Meneja msaidizi wa Castle Lite, Victoria Kimaro akizungumza katika uzinduzi wa kampeni ya shindano la Lite Up The Weekend ambapo washindi watajipatia VIP tiketi ya kushiriki katika Yacht Party. Katikati ni Meneja wa Castle Lite Geofray Makau na pembeni ni meneja masoko wa Castle Lite Vimal Vaghmaria.
Wanahabari wakielekea eneo la maegesho ya Yacht itakayotumika katika kilele cha cha kampeni ya Lite Up The Weekend.

Muonekano wa Yacht itakayoandaliwa maalum kwa ajili ya washindi wa shindano la Lite Up the weekend.
Mmoja ya wadau wadau wa Castle Lite katika pozi ndani ya Yacht.


Meneja masoko wa Castle Lite Vimal Vaghmaria na Stanley Kafu wa Aggrey & Clifford wakifurahia ndani ya Yacht.

Wanahabari katika pozi la pamoja na wadau wa Castle Lite.
 Waandishi Tukijiachia kupata raha.

Na Mwandishi Wetu

KAMPUNI ya Bia Tanzania kupitia kinywaji chake cha Castle Lite, jana imezindua rasmi promosheni kubwa itakayojulikana kama ‘Lite Up The Weekend’, huku Watanzania wakipewa nafasi ya kujishindia zawadi mbalimbali.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Meneja wa Bia ya Castle Lite, Geoffrey Makau, alisema nia kubwa ni ya kufanya hivyo ni kutaka kuwaweka Watanzania pamoja.

Alisema, promosheni hiyo itaendeshwa nchi nzima, kupitia katika kifuniko cha bia ya Castle Lite, huku kukiwa na zawadi mbalimbali zitakazotolewa kila wiki, ikiwa ni fedha taslimu, vifaa vya kusikilizia muziki na nyingine nyingi.
 Waandishi wa Habari wakipelekwa kisiwani kwenda kupanda boti ambayo washindi watapelekwa kula raha.
Kapteni wa Boti akitoa maelezo kwa waandishi wa habari pamoja na wafanyakazi wa TBL.
 Waandishi wakiwa na wafanyakazi wa TBL wakifurahia ndani ya boti yetu.

“Ila zawadi kubwa zaidi ni ile ya washindi kupata fursa ya kufanya sherehe kubwa ndani ya boti ya kifahari, sherehe hii itajulikana kama ‘Castle Lite VIP Yacht Party’,” alisema Makau.

Meneja huyo alisema, sherehe hii itakayoanzia ndani ya boti, itaishia katika kisiwa cha Sinda kilichopo katikati ya Bahari ya Hindi jijini Dar es Salaam, ambapo muziki, vyakula na vinywaji vitakuwa vimeandaliwa kwa ajili ya washindi hao toka mikoa mbalimbali ya Tanzania.

Alisema, mteja atatakiwa kununua bia ya Castle Lite ya chupa yenye ujazo wa mililita 375 au 330 na kuangalia ndani ya kifuniko, ambapo atakuta namba za siri, kisha atatuma namba hizo kwenda 15499 au kutembelea tovuti ya www.castlelite.co.tz ili apate nafasi ya kushinda zawadi za kila wiki au zawadi kubwa ya ‘Castle Lite Yacht Party’.
 Shangwe.
 Mmilikiwa wa Kajunason Blog, Cathbert Kajuna akiwa na Meneja msaidizi wa Castle lite Tanzania, Victoria Kimaro ndani ya visiwani wakipata raha ndani ya boti.

Aidha kutakuwa na zawadi za kila siku kupitia vituo vya radio, ambapo wapenzi wa Castle Lite wakipiga simu watatakiwa wapokee kwa kuanza na neno ‘Lite Up The Weekend’ na wateja watakaofanya vizuri watapata zawadi mbalimbali.

Mbali na zawadi, wale washindi watapata nafasi ya kuhudhuria matamasha mbalimbali ya muziki hapa nchini.

“Ninawaomba wapenzi wa bia hii ya Castle Lite, kushiriki mara nyingi wawezavyo ili kushinda zawadi hizi za kuvutia,” alisema Makau.

Castle Lite ni kinywaji kinachozalishwa na kusambazwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), iliyo na nguvu kubwa ya soko hapa nchini.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>