Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakitembelea Maktaba ya Kirais ya Rais Bush (Bush Presidential Library) na kujionea nafasi kubwa iliyotolewa kwa Tanzania na zawadi ambazo Rais Bush alizipata katika ziara yake rasmi ya Tanzania wakati akiwa Rais wa Marekani. Maktaba hiyo ya kuvutia inaendeshwa kwa teknolojia ya kisasa kabisa ya habari na mawasiliano.
Rais Kikwete alikuwa amesimama mjini Dallas kwa muda akiwa njiani kutoka Washington D.C., kwenda Houston, jimbo hilo hilo la Texas kuhudhuria mkutano wa wafanyabiashara wa mafuta na gesi ambao wanataka kuwekeza katika sekta hiyo katika Tanzania.
Rais Kikwete amekuwa katika Marekani kwa ziara ya kikazi ya siku tisa, ambako miongoni mwa mambo mengine, amehudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Marekani na Afrika uliofikia kilele chake jana kwa kikao kilichoendeshwa na Rais Barack Obama wa Marekani katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani mjini Washington D.C.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakitembelea Maktaba ya Kirais ya Rais Bush (Bush Presidential Library) sehemu ambayo imejengwa kwa mfano wa Ikulu ya Marekani, White House, hususan katika bustani y a Waziri (Rose Garden) pamoja na ofisi ya Rais wa Marekani, Oval office
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakitembelea na kujionea vitu mbalimbali ambavyo Rais mstaafu George W. Bush alipewa kama zawadi kutoka Tanzania ambavyo vimehifadhiwa katika Maktaba ya Kirais ya Rais Bush (Bush Presidential Library)
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakitembelea sehemu ya mfano wa ofisi ya kupangia mikakati ya Ikulu ya Marekani iliyotumika na Rais MStaafu George W. Bush kwenye Maktaba ya Kirais ya Rais Bush (Bush Presidential Library)
PICHA NA IKULU