''(Sina maneno ya kusema zaidi ya kumshukuru Mungu kwa uponyaji wake, pia nawashukuru watu wote walioniombea pamoja na waliokuja kuniona hata wale ambao wameshindwa kufika, kwani najua walikuwa wakiniombea)''
Hayo ni baadhi ya maneno ya muimbaji wa nyimbo za injili Bahati Bukuku, akiieleza GK, kutokana na ajali aliyopata usiku wa kuamkia tarehe 26 Julai 2014.
GK ilifika nyumbani kwake Tabata kwa mara nyingine kwenda kumjulia hali, ambapo ilimkuta Bahati Bukuku akiwa mzima wa afya njema huku akiwa amejipumzisha kwenye godoro sebuleni kwake.
GK ilitaka kujua kama kwa sasa anaweza kuinuka na kutembea mwenyewe bila kusaidiwa na mtu yoyote, ndipo hapo Bukuku akaamua kuionyesha GK kwa vitendo kwa kuamka mwenyewe na kutembea kisha kurudi tena sehemu alipokuwa amepumzika.