Meneja wa huduma wa Benki ya NMB tawi la Mwanjelwa Jijini Mbeya, Happnes Pima (kulia) akimwelekeza jambo Mkuu wa Wilaya ya Wangi'ombe Mkoa wa Njombe, Estelina Kilasi (kushoto) wakati alipotembelea banda ya benki hiyo kwenye maonyesho ya wakulima ya nanenane yanayoendelea kwenye viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya, ambapo kwa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini yanafanyikia Mkoa wa Mbeya.
Meneja wa huduma wa Benki ya NMB tawi la Mwanjelwa Jijini Mbeya, Happnes Pima (katikati) akimwelekeza jambo Mkuu wa Wilaya ya Wangi'ombe Mkoa wa Njombe, Estelina Kilasi (kushoto) wakati alipotembelea banda ya benki hiyo kwenye maonyesho ya wakulima ya nanenane yanayoendelea kwenye viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya, ambapo kwa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini yanafanyikia Mkoa wa Mbeya.
Askari wakiwa wameimarisha ulinzi kwenye banda ya benki ya NMB katika maonyesho ya wakulima ya nanenane yanayoendelea kwenye viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya, ambapo kwa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini yanafanyikia Mkoa wa Mbeya
Wafanyakazi wa Benki ya NMB wakiwajibika katika banda lao kwenye maonesho ya wakulima maarufu kama Nanenane ambayo kwa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini yanafanyikia Mkoa wa Mbeya, katika Viwanja vya John Mwakangale Jijini Mbeya.
Baadhi ya askari polisi wakipewa maelezo ya namna ya kuchukua mikopo kutoka Benki ya NMB na Ofisa Mikopo Shekha Diwani, askari hao walitembelea kwenye banda la NMB jana lililomo Viwanja vya Maonyesho ya Nane Nane yanayoendelea jijini Arusha eneo la Njiro.
---
Na Mwandishi Wetu.
Benki ya NMB inashiriki maonyesho ya wakulima ya nanenane katika mikoa saba huku huduma zote za kibenki zikiwa zinafanyakazi katika mabanda yake kama kuweka na kutoa fedha, kupata taarifa za mikopo hasa ya kilimo.
NMB inashiriki maonyesho ya nane nane katika mikoa ifuatayo; Lindi ambako yanafanyika kitaifa, Morogoro, Dodoma, Tabora, Mbeya, Arusha na Kagera.
Wakulima pia wanaotembelea mabanda ya NMB kote nchini watapata fulsa ya kukutana na wataalam wa kilimo na pembejeo, vyama vya ushirikana hivyo kuwa na fulsa nzuri za wao kupata taarifa sahihi na ushauri wa jinsi ya kutumia benki kunufaisha shughuli zao za kilimo.
Kwa kuwa moja ya malengo ya NMB ni kuhakikisha inasaidia ukuaji wa kilimo na kukifanya kuwacha kibiashara, yenye malengo la kumkwamua mkulima. Hii ni fursa nzuri kwa wakulima, wafanyakazi wa serikali na wajasiriama likuweza kufika kwenye mabanda ya NMB ilikujionea huduma ambazo benki inatoa.
Kilimo ni uti wa mgongo kutokana na ukweli kwamba karibia 80% ya watanzania wanajishughulisha na kilimo. Kwa kutambua hilo, NMB ipo karibu yao zaidi katika kipindi hiki cha Nane Nane kwa kuleta huduma za kuwanufaisha.
Kauli mbiu ya‘Kilimo na Mifungo ni biashara’ kwa mwaka huu imeifanya NMB kushirikiana na serikali katika kufanikisha maonyesho ya nanenane katika mikoa yote saba.
Benki ya NMB inatoa huduma mbalimbali za kilimo ikiwa ni pamoja na akaunti maalumu ya Kilimo yaani ‘Kilimo Account’ ambayo inamruhusu mkulima kuweza kujipatia mikopo mbalimbali ilikuweza kuinua uchumi wa Nchi.