Mlipoanza Mapenzi, kwenda Dodoma kumsalimia Honey haikuwa shida, kwakuwa ilikuwa mwanzo na si ajabu hata tunda ulikuwa hujapewa... Ulionyesha kweli jitihada na mahaba na kumfanya mpenzi wako ajihisi yeye ameokota Malaika katikati ya Vibwengo.
Ila sasa... Baada ya miezi kadhaa au mwaka mmoja kupita, akikwambia mpenzi njoo nimekumiss unahisi Dodoma ni mbali kama Afghanistan... Mara oh! nna workshop wiki hii nzima, Mara Niko Tight na Month end reports...
Kuna Auditors ofisini.... Nina mitihani inakuja na assignments.. Sababu kibao?? Nini kimetokea?? Si ni wewe uliyemuahidi kwamba Distance doesn't matter? Tena ukamsisitizia hadi kidevu kikakucheza na ndevu kukusimama, mtoto akaingia laini, ukamuonjesha Mahaba ya Probation, akaishi kama Malkia ile miezi 6 ya Kwanza, kwenda Dodoma haikuwa shida kama Mbunge vile...
Poleni sana wale mlio kwenye Long Distance Relationship, uko Dar yeye Arusha lakini utadhani yuko Urusi, mnaonana kwa nadra kuliko Jua kukutana na Mwezi jioni kumbe wote mko Tanzania hii hii... Ukijijua huwezi Long distance Relationship USIINGIE. Mapenzi haya yanataka Commitment, yanataka Kujitoa... Yanataka Sacrifice... Wengi mmeahidi lakini hamtendi... Na mlioahidiwa mmebaki mnalia, Akijitahidi sana atakupa Mapenzi ya Skype, sasa sijui na watoto mtatafutia Skype???
Imeandikwa na Seth Giovanni, Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Mapenzi.