Rais wa Marekani, Barack Obama akinyanyua glass yake juu wakati alipowaandalia chakula cha usiku marais kutoka mataifa mbalimbali Barani Afrika katika ikulu ya Marekani, White House jana usiku.
Rais Obama aliandaa dhifa hiyo baada ya kumalizika kwa mkutano wa siku tatu uliokuwa na lengo la kuimarisha ushirikiano kati ya Marekani na mataifa ya Afrika.
Mwanamuziki Lionel Richie akitumbuiza katika dhifa hiyo iliyoandaliwa na Rais Barack Obama wa Marekani kwa marasi mbalimbali toka Barani Afrika iliyofanyika katika Ikulu ya Marekani, White House jana usiku
Rais wa Gambia, Yahya Jammeh akiwasili ikulu ya Marekani akiwa ameongozana na mkewe Zinneb Jammeh.
Rais wa Burkna Faso, Blaise Compaore akiwasili Ikulu ya Marekani kuhudhuria dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa na Rais wa Marekani, Barack Obama jana usiku.
Rais wa Cameroon, Paul Biya akiwa ameongozana na mkewe Chantal Biya wakiwasili White House.
Rais wa Rwanda, Paul Kagame akiwa ameongozana na mtoto wake Ange Ingabire Kagame wakiingia Ikulu ya Marekani.
King Mswati III wa Swaziland akiwa na mkewe Inkhosikati La Mbikiza wakiingia White House kuhushuria pamoja na viongozi wengine wa Afrika dhifa maalum iliyoandaliwa na Rais Obama.
Rais wa Malawi, Peter Mutharika akiwapungia mkono waalikwa wengine waliohudhuria dhifa maalum iliyoandaliwa na Rais Obama. Zaidi ya waalikwa 400 walihudhuria.
Mke wa Rais wa Marekani, Michelle Obama akirejea katika kiti chake baada ya kusalimiana na waalikwa mbalimbali waliofika katika dhifa hiyo.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerry ( kushoto ) akibadilishana mawazo na Rais wa zamani wa taifa hilo, Jimmy Carter