Mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe mchana wa leo Agosti 5, 2014 amewatimua wakuu wa Idara 6 waliokuwa katika ziara yake eneo la Mlangali kwa kuwataka wakafuate vitanda vinne vya zahanati ya Mlangali ambavyo alivinunua yeye na halmashauri kuendelea kuviweka stoo huku wagonjwa wakilala chini japo fedha za kusafirisha vitanda alizitoa zaidi ya miezi miwili sasa.
Pia wananchi wa kijiji cha Mlangali wampongeza mbunge wa jimbo lao kwa kuwatimua wakuu wa Idara kwa kuonyesha uzembe, mbali ya vitanda hivyo mbunge adai amevinunua mwaka mmoja uliopita Vipo stoo hadi Leo mbali ya vitanda pia alikabidhi GARI ya wagonjwa ambayo hadi Leo matengenezo mbali mbali anafanya kwa gharaza zake