Quantcast
Channel: HABARI NA MATUKIO
Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

BILIONI 1.6 ZINAHIAJIKA ILI KUWAWEZESHA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU KWENDA MAFUNZO KWA VITENDO

$
0
0
Zaidi ya shilling billion 1.6 zinahitajika kwa wanafunzi wa elimu ya juu nchi katika kukamilisha sehemu ya masomo ambayo ni mafunzo yao kwa vitendo ambapo hadi sasa hawajaweza kuripoti katika sehemu walizopangiwa.

Akizungumza jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Jumuiya ya wanafunzi wa elimu ya juu (TAHLISO) Mussa Mdede amesema kwamba ni wiki ya nne tangu mafunzo hayo yaanze lakini hadi sasa vyuo vipatavyo saba havijaweza kupata fedha za mafunzo ambapo bado jitahada walizofanya hazijaweza kuza matunda mazuri.

Aidha Mdede amesema kwamba hadi sasa serikali haijatoa tamko lolote kuhusiana na hilo ambapo madhara makubwa yanaweza kutokea kama mwanafunzi hajafanya sehemu hiyo ya mafunzo na wameendelea kufatilia katika bodi ya mikopo wameambiwa bado hawajapokea fedha toka hazina.

Wakati huo huo Mwenyekiti huyo ametoa onyo kwa wanasiasa wanaotumia jumuiya hiyo kwa manufaa yao binafsi ambapo waowapo kwa ajili ya kutetea maslahi ya wanafunzi wa vyuo vikuu na si siasa.

Hata hivyo ameisihi serikali kujitahidi kuchukua hatua za haraka hadi ifikapo wiki ijayo kwani baada ya hapo wao wamejipanga kuchukua hatua nyingine zaidi ilikulipataia ufumbuzi jambo hilo.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

Trending Articles