Mchekeshaji Anne Kansiime amewasili leo Julai 31, 2014 jijini Dar es Salaam tayari kwa burudani kali hapo August 2 kwenye ukumbi wa Golden Tulip. Mkali wa huyo wa kuchekesha na sanaa za majukwaani Afrika Mashariki, amewasili majira ya saa kumi jioni kwa ndege ya shirika la Rwanda.