Brand Manager wa Kampuni ya Tigo, Bw. William Mpinga akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam juu ya Tamasha la muziki la TABASAMU litakalofanyika kwenye fukwe za Coco Beach jijini Dar es salaam tarehe 10.2.2013.
Mwakilishi wa Kampuni ya Prime Time Promotions ambao ni waandaaji tamasha hili la Tigo, Bw. Lumuliko Mengere a.k.a Mully B akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari kuhusu tamasha kubwa la Muziki kuzindua msimu wa Tabasamu na Tigo! Pembeni yake ni Brand Manager wa Kampuni ya Tigo, Bw. William Mpinga.
Msanii wa kizazi kipya Chege akitoa kionjo mbele ya waandishi wa habari. Kushoto ni Meneja wa kundi la TIP TOP Connection, Babu Tale na pembeni ni Meneja wa kundi la Wanaume TMK, Said Fela.
Msanii wa kizazi kipya, Mr. Blue akiongea machache katika mkutano wa waandishi wa habari kudhibitisha ushiriki wake katika tamasha hilo.
---
Tigo Tanzania inapanga kufanya tamasha kubwa la kuzindua msimu wa Tabasamu ambao umetokana na Tigo kubadilisha kauli mbiu yake ya zamani kutoka Jielezee mwenyewe” kuwa “Tabasamu! upo na Tigo”.
Meneja wa chapa ya Tigo Bwana William Mpinga alielezea kuhusu uzinduzi huo akisema “Tigo ina fahari kubwa kwa jinsi ambavyo inawajali na kuwapa thamani wateja wake kupitia bidhaa zake mbalimbali za mawasiliano. Mabadiliko haya ya kauli mbiu yanatupa fursa ya kuonyeshadhamira yetu ya kuwajali Watanzania pamoja na kuwahakikishia kwamba tutakuwa nao sambamba kwa kila jambo, wakati wote. Wateja wetu ni msukumo wa kila tufanyacho Tigo, hivyo tunajitahidi kuhakikisha tunawatimizia mahitaji yao yote ya mawasiliano. Lengo letu linabakia kujenga na kutoa huduma za unafuu , zinazopatikana kila mahali na kwa wote.”
“Uzinduzi wa msimu huu wa Tabasamu unalengo la kuhakikisha watu wengi zaidi wanatabasamu kutokana na bidhaa zetu zenye thamani, mtandao wenye ubora wa juu na huduma nzuri kwa wateja kama ishara ya shukrani kwa nafasi yetu muhimu kwenye maisha ya Watanzania. Tumekuwa ni sehemu ya maisha yako na tunataka kuwa na wewe siku zote hivyo Tabasamu, upo na Tigo! ” Alihitimisha Bwana Mpinga.
Tamasha hili litafanyika katika ufukwe wa Coco (Coco Beach) Jumapili ya tarehe 10 Februari 2013 kutoka saa 7:00 mchana hadi saa 12:00 jioni na litashirikisha burudani kali kutoka kwa Enika, Roma Mkatoliki, TMK Wanaume, Tip Top Connection, Juma Nature, Recho, Mr. Blue na wachezaji dansi wa THT .
Mtaalamu wa Biashara na Masoko wa Tigo bwana Alex Msigara alisema juu ya tamasha kwamba “ukiachana na burudani kutoka kwa wanamuziki hao mahiri vilevile kutakuwa na zawadi kubwa za kushindaniwa na promosheni na ofa za kusisumua. Tutakuwa na bidhaa na huduma mbalimbali za ofa za Tigo hivyo tunatarajia ujio mkubwa na tunawahakikishia burudani kali ya kuanza mwaka na tabasamu”
Msimu huu wa tabasamu unahusisha ofa, promosheni, zawadi na bidhaa mbalimbali za thamani kutoka Tigo ambazo zitawalenga wateja wa vipengele vyote na mahitaji yao yote.