Na Hellen Kwavava wa Kajunason Blog, Dar es Salaam.
Zaidi ya watoto 37 wamezaliwa katika mkesha wa kuamkia Idi Al fitri jijini Dar es Salaam ambapo saba kati yao wamezaliwa kwa operesheni kutokana na wazazi wao kuwa na matatizo kabla ya kujifungua.
Watoto hao sita wametokea hospitali ya Taifa Muhimbili na 31 wametokea hospitali ya Amana ya jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na Kajunason blog, Kaimu mkuu muuguzi wa hospitali ya Muhimbili Sista Jane Chuwa amesema kwamba wazazi wengi wanao kuja kujifungulia hapo wanakuwa wametoka hospitali nyingine kutokana na kuwa na matatizo ya uzazi.
Naye afisa Muuguzi wa hospitali ya amana Sista Neema Mbafu ameeleza kuwa watoto 18 ni wakiume na 13 wakike ambapo idadi ya watoto waliozaliwa leo imepungua ukitofautisha na siku nyingine ambapo kwa siku wanazalisha wazazi zaidi ya 60.
Hata hivyo wauguzi hao wamesema kuwamba wanakabiliwa na changamoto kubwa wa wauguzi kwani wao wapo wachache na wengi wakiajiriwa wanakaa kwa muda na kuondoka kutokana na kazi kuwa nyingi.