Quantcast
Channel: HABARI NA MATUKIO
Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

NAKUMATT YAFUNGUA TAWI LA KWANZA DAR ES SALAAM, YAPANGA KUFUNGUA MENGINE MAWILI

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Nakumatt Holdings, Atul Shah akimuonesha baadhi ya bidhaa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Janet Mbene wakati wa ufunguzi huo leo
 Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Janet Mbene akiangalia bidhaa wakati wa ufunguzi huo leo.

Wafanyakazi wa Nakumatt Mlimani wakifurahia wakati wa sherehe za ufunguzi wa mall hiyo Mlimani City jijini Dar es salaam leo
Furaha ya kuanza kazi Nakumatt Mlimani leo.

Na Mwandishi Wetu.

KAMPUNI ya Nakumatt Holdings, imezindua rasmi tawi la kwanza kati ya matawi yake matatu makubwa nchini Tanzania ambayo awali yalimilikiwa na Kampuni ya Shoprite ya Afrika ya Kusini. 

Ikiwa ni mpango wake mpya wa kuboresha zaidi huduma zake, Nakumatt holdings, imezindua tawi hilo kubwa ambalo litakuwa utambulisho muhimu wa huduma zake katika eneo la biashara la Mlimani City litakaloitwa Nakumatt Mlimani. 

Tawi hilo la 48 la Nakumatt limepambwa kwa rangi na mwonekano wa alama za Nakumatt na kwa ubunifu wa hali ya juu.

Pamoja na Nakumatt Mlimani, kampuni hiyo pia iko mbioni kuzindua tawi lengine kubwa litakalojulikana kama ‘Nakumatt Pugu Road’ jijini Dar es salaam ambako pia kutakuwa makao yake makuu. Pia itafungua Nakumatt Arusha siku zijazo. 


 Kwa kufungua matawi yake matatu moja baada ya jingine, Nakumatt pia itakuwa imefikisha matawi 50 katika mtandao wake wa huduma za uuzaji bidhaa na hivyo kutekeleza mkakati wake wa maendeleo ambao ulizinduliwa mwaka 2011.

 Akizungumza wakati wa uzinduzi wa duka lake la kwanza in Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Nakumatt Holdings, Atul Shah alisema kufunguliwa kwa matawi matatu mapya yaliogharimu takriban dola za Marekani milioni 3 ni sehemu ya mpango wa upanuzi wa huduma za uuzaji bidhaa katika kanda ya Afrika.

Kutokana na uzinduzi wa Tawi la Nakumatt Mlimani, Shah alisema kuwa Nakumatt sasa ina maduka mawili makubwa yanayofanya kazi nchini Tanzania. 


Nakumatt Mlimani inaungana na duka jingine la la Nakumatt Moshi lililofunguliwa mwaka 2011 katika mji huo ambako kuna Mlima Kilimajaro. 
”Uzinduzi wa Nakumatt Mlimani ni ndoto ya muda mrefu ambayo sasa imekuwa kweli ambapo tumekuwa tukifikira mahali pa kuweka duka letu jijini Dar es salaam na maeneo mengine nchini Tanzania,” alisema Shah na kuongeza:

“Uzinduzi huu pia ni hatua nzuri itakayopelekea uzinduzi mwingine wa duka letu la 50 katikati ya Agosti ambapo tutakuwa tumefanikiwa kufikia malengo yetu tuliyojiwekea kuyafikia Februari mwakani.”


Maduka matatu ya Shoprite yalifungwa mwezi uliopita ili kufanikisha kazi ya kuyaboresha zaidi sambamba kwa kuzingatia viwango na uzoefu wa Nakumatt. 


Pia Nakumatt inatarajia kufungua matawi mengine matatu ya biashara nchini Kenya kabla ya mwisho wa mwaka huu.

 Pia kampuni hiyo itakuwa na duka kubwa katika eneo kubwa la kifahari la Green Square mjini Kericho nchini Kenya.

Shah alisema Nakumatt ina mkakati wa kukuza biashara wa kampuni ambao unategemea zaidi uwepo wa vitega uchumi ambapo kampuni inaweza kuendesha shughuli zake za maduka ya supermaketi. Shah aliongeza kwa kusema:


 “ Kwa sasa tunaendesha shughuli zetu katika nchi 12 na tunashirikiana na wamiliki wa maeneo ya biashara nchini Kenya ambao wanaweza kutoa huduma za kujenga maeneo ya maduka makubwa katika maeneo ya Machakos, Nyeri, Kajiado, Garissa, Embu, Naivasha,Narok Busia and Homabay.” 

Ili kutimiza masharti ya Nakumatt, Shah aliwahimiza waendelezaji wa maeneo ya biashara na Mameneja wa Miradi kushauriana na wataalam wa Nakumatt kuhusu namna ya kuboresha uchoraji wa ramani na ujenzi wenye mvuto kwa wateja katika maduka ya kampuni hiyo.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>