Quantcast
Channel: HABARI NA MATUKIO
Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

WATU WA MAREKANI WAUNGANA NA WATANZANIA KUWASAIDIA WATOTO KATIKA MAZINGIRA HATARISHI

$
0
0
Tarehe 1 Februari, mjini Dodoma, Tanzania ilizindua Mpango Kazi wa Awamu ya Pili wa Kitaifa wa Huduma kwa Watoto walio katika Mazingira Hatarishi unaofadhiliwa na watu wa Marekani kwa kupitia Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) kwa ubia na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii. 

Mpango huu ulizinduliwa na Waziri Mkuu Mheshimiwa Mizengo Pinda kwa niaba ya Serikali ya Tanzania. Kuzinduliwa kwa mpango huu ni ishara ya dhamira ya dhati ya Serikali ya Tanzania, watu wa Marekani na wabia wengine wa maendeleo katika kuboresha maisha ya watoto wa Tanzania walio katika mazingira hatarishi.

Janga la VVU/UKIMWI limeongeza idadi ya watoto walio katika mazingira hatarishi. Ili kukabiliana na Changamoto hii kikamilifu, USAID ikiwa sehemu ya Mpango wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kukabiliana na VVU/UKIMWI (PEPFAR) ilishirikiana na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kuandaa Mpango Kazi wa Kwanza wa Kitaifa wa Huduma kwa Watoto walio katika Mazingira Hatarishi wa mwaka 2007 hadi 2010. Hali kadhalika, USAID ilisaidia mfumo wa kwanza kabisa wa kitaifa wa usimamizi wa takwimu kuhusu watoto walio katika mazingira hatarishi (Most Vulnerable Children Data Management System) ambao unafuatilia utekelezaji wa mpango kazi.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mpango huu, Afisa Afya wa USAID Andrew Rebold alisema kuwa, “Kwa watoto walio katika mazingira hatarishi mliohudhuria hapa leo, tungependa mfahamu kuwa Marekani inashirikiana na Tanzania katika kuyafanya maisha yenu ya baadaye kuwa bora zaidi.”

Ubia kati ya USAID na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii uliwezesha kutekelezwa kwa Mpango Kazi katika halmashauri 95 kati ya 133. Hadi kufikia mwezi Septemba 2012, zaidi ya watoto 269,000 walio katika mazingira hatarishi walikuwa wamepatiwa huduma mbalimbali na zaidi ya kaya 50,000 zenye watoto walio katika mazingira hatarishi ziliweza kuongeza kipato chao. Jitihada hizi ziliwezeshwa pia na ushiriki wa mashirika yasiyo ya kiserikali, vikundi vya kijamii na taasisi za kidini.

Ili kuhakikisha utekelezaji wenye mafanikio wa Mpango Kazi mpya, USAID itasaidia katika kuimarisha uratibu na usimamizi wa utekelezaji huo. Aidha, USAID itasaidia katika kuandaa mkakati wa mawasiliano ili kuhakikisha kuwa mpango huu unasambazwa kwa wahusika wote na huduma stahili zinawafikia walengwa. Hali kadhalika, itasaidia kuimarisha uwezo wa idara na vitengo vya serikali vinavyoshughulikia ustawi wa jamii wa kutoa huduma na ulinzi kwa watoto. Hii itajumuisha kuimarisha watendaji wa idara ya ustawi wa jamii katika ngazi zote.

Inakadiriwa kuwa asilimia 10 ya watoto wote hukabiliwa na Changamoto za kijamii, kiuchumi na kisaikolojia zinazoweza kuwaingiza katika mazingira hatarishi. Hizi ni pamoja na umasikini; kufiwa kwa wazazi au walezi wao; kutelekezwa; kunyanyaswa kutokana na kukosa ulinzi na kutokupata matunzo na huduma nyingine za msingi. Katika kipindi cha miaka 10 iliyopita, USAID kwa kupitia PEPFAR imekuwa ikisaidia jitihada za kurefusha maisha ya watu wanaoishi na VVU kwa kutoa dawa za kupunguza makali ya virusi hivyo(ARVs), kusaidia programu ya kuzuia maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto, na kusaidia kupunguza maambukizi mapya kuwa kutoa huduma za kinga na elimu

Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

Trending Articles