Mwanamke wa Sudan aliyenusurika hukumu ya kifo nchini mwake kutokana na kuukana Uislam amesafirishwa kwa ndege hadi Italia baada ya kukaa kwa zaidi ya mwezi mmoja kwenye ubalozi wa Marekani huko Khartoum.
Meriam Yahia Ibrahim Ishag pamoja na familia yake walipokelewa Roma na Waziri Mkuu wa Italia, Matteo Renzi, ambaye alisema leo ni siku ya kusherehekea.
Baba wa Meriam ni muislam mama mkristo na kwa mujibu wa sheria za Kiislam mwanamke huyo alipaswa kuwa muislam na hakutakiwa kubadili dini na kuwa mkristo.