




Na Hellen Kwavava wa Kajunason Blog.
Zikiwa zimebaki siku 12 kwa bunge maalum la katiba kuanza tena wajumbe wanawake wa bunge hilo pamoja na mtandao wa wanawake na katiba na Tamwa wamekutana leo jijini dar es salaam ili kujadili mchakato mzima wa katiba hususani haki ya mwanamke katika usawa wa jinsia na katiba.
Akizungumza mara baada ya kufungua mkutano huo Mkurugenzi wa TAMWA Valeria Msoka amesema kwamba wao wanahitaji katiba itakayo zingatia jinsia na si kuegemea upande mmoja na pia itaangalia kwa umakini na kutoa kipaumbele masuala ya wanawake.
Naye Mwenyekiti wa Mtandao wa wanawake na katiba, Mary Lusinde ameeleza kwamba wanatarajia mambo waliyoyajadili katika mkutano huo yatafanyiwa kazi katika katiba mpya ambapo masuala yote yanayodai sheria kubadilishwa ili katika chaguzi zote zinazokuja ziwe na msingi huo wa kulinda utu wa mwanamake na mtoto.
Mmoja wa wajumbe wabunge la katiba ambaye pia mbunge wa zanzibar kupitia jimbo la wete Mbaruku Salim Ali amesema kwamba katiba ya zamani haikutoa fursa kwa wanawake kwasasa ipo haja ya kuhakikisha haki inapatikana kwa mwanamke na mtoto.
Hata hivyo wadau mbalimbali wameweza kutoa ushauri kwa wajumbe hao wanawake kuweza kuondoa aibu pindi wanapohitaji haki zao ili utekelezaji wa haraka na umakini ufanyike haraka na mapema.