Picha/Habari na Mdau wa Kajunason Blog, Bw. Ochu Kunambi, Lindi
Walinzi wawili Ambao walikuwa walinzi wa Kituo cha Mafuta cha Kobil kilichopo Mnazi mmoja Kata ya Mingoyo Manispaa ya Lindi wameuawa na watu wanaodhaniwa kuwa majambazi ambapo walifanikiwa kuvunja kituo hicho lakini walishindwa kupata fedha baada ya kushindwa kuvunja/kubeba (self) huku wakiitelekeza kichakani bunduki aina ya Short Gun ya walinzi hao.
Tukio hilo limetokea ikiwa ni mfululuzo wa mauaji ya walinzi wa vituo vya mafuta yaliyotokea siku za hivi karibuni, Tukio limetokea Usiku wa kuamkia leo na kubainika asubuhi baada ya Meneja wa kituo hicho ,Bw Saidi Ally Rashid kukuta walinzi hao wakiwa wamelala wakivuja damu
Walinzi hao waliopigwa na kufariki papo hapo walifahamika kwa jina la Selemani Mohamed Mchawi na Mohamed Twalib wote wakiwa ni wakazi wa Mingoyo.
Akizungumza na Waandishi wa Habari waliofika eneo la tukio, Meneja wa Kituo hicho cha Mafuta cha Kobil, Saidi Ally Rashid Alibainisha kuwa majira ya saa 12 Asubuhi alifika hapo kituoni kama ilivyo kawaida huwakuta walinzi na kumkabidhi kituo‘
Waandishi yaani leo nimeona ajabu nafika simuoni hata mlinzi mmoja nikiangalia mlango wa Shell uko wazi kioo kimevunjwa… Nilipozunguka zaidi nilikuta walinzi wakiwa wamelala wakivuja damu na Kwa Ishara nilibaini wamekufa.. Nilishtuka sana na nilikimbilia kituo cha Polisi kwa taarifa zaidi ya nilichoona asubuhi hii’ Alimalizia Said.