Komweta Hemed Maneti a.k.a Chiriku mwanamuziki wa bendiya Vijana Jazz.
Marehemu Hemedi Maneti Ulaya Chiriku aliyekuwa mwamuziki wa bendi ya Vjana Jazz enzi hizo.
---
Komweta Hemed Maneti a.k.a Chiriku ni Mtoto wa mwanamuziki wa zamani marehemu Hemedi Maneti Ulaya Chiriku aliyekuwa akiimba katika bendi ya umoja wa vijana Vijana Jazz enzi hizo ambapo anasema amekuwa kwenye muziki kwa muda mrefu japokuwa kama ilikuwa kama kujifurahisha, Komweta Hemed Maneti alianza muziki kama kazi mwezi Agosti mwaka 2013 akiimba katika bendi ya Vijana Jazz ambayo marehemu baba yake Mzee Hemedi Maneti Ulaya aliitumikia kwa mafanikio enzi za uhai wake.
Komweta Hemed Maneti a.k.a Chiriku amekuwa akijizolea umaarufu mkubwa katika bendi hiyo kwani mashabiki wengi wamekuwa wakimkumbuka marehemu baba yake mara anapoimba jukwaani kwani kwa kiasi kikubwa sauti zinaendana na marehemu baba yake Hemed Maneti, Bendi ya Vijana Jazz imekuwa ikipata umaarufu siku hadi siku katika maonyesho yake yanayofanyika kwenye klabu ya Kilwa Road Pub Ijumaa, Jumamosi wanapiga Jet Lumo na Jumapili kwenye ukumbi wa Vijana Hall Kinondoni.
Wanamuziki wakongwe waliobaki kwenye bendi ya vijana Jazz ambao waliwahi kuimba na marehemu Hemed Maneti ni Shomary Ally, Abdallah Mgonahazeru na Roshy Mselela, Ndoto za Komweta Hemed ni kuwa mwanamuziki wa kimataifa na kuipepeprusha vema bendera ya Tanzania ndani na nje ya mipaka ya TANZANIA ameolewa na ana mtoto mmoja wa miaka 5 anayeitwa Fahad.
Anaongeza kuwa Changamoto za kazi ya muziki na malezi ni nyingi lakini muhimu ni kujua jinsi gani utapanga ratiba zako vizuri na kuhakikisha unafanya maandalizi mazuri kwa ajili ya mtoto na hili halinishindi natimiza majukumu yangu vizuri kama mama.
Anaongeza kuwa Changamoto za kazi ya muziki na malezi ni nyingi lakini muhimu ni kujua jinsi gani utapanga ratiba zako vizuri na kuhakikisha unafanya maandalizi mazuri kwa ajili ya mtoto na hili halinishindi natimiza majukumu yangu vizuri kama mama.
hata hivyo siku za jumatatu zinakuwa zina changamoto kubwa sana hasa katika kumwandalia mahitaji yake kwa ajili ya kwenda shule kwakuwa nakuwa nimechoka na kazi.
Mwanamuziki huyo anasema mashabiki wa bendi ya vijana wamempokea vizuri sana kusema kweli anaongeza kuwa "Nashukuru Mungu sana kwa hilo na hili linajidhihirisha ninapokuwa nafanya shoo zangu...watu hawakai chini mara nyingi wanakuwa wakicheza..."
Anamaliza kwa kusema "Umaarufu wa marehemu baba yake mzee Hemed Maneti upo na siwezi kuuepuka...lakini kubwa watu wananipima kutokana na utendaji na ufanisi wangu wa kazi yangu niwapo jukwaani".