Quantcast
Channel: HABARI NA MATUKIO
Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

AIRTEL YATOA MSAADA WA VITABU VYA SHILINGI MILIONI 9 KWA SHULE ZA SEKONDARI KAGERA

$
0
0
 Toka kulia ni Afisa Mauzo wa Airtel Kagera bw Leonard maige na Meneja
mauzo wa kampuni ya Airtel wa mikoa ya Kagera na kigoma bw. Peter Kimaro katikati wakikabidhi sehemu ya vitabu vya sekondari vya masomo ya sayansi kwa afisa elimu wa shule za sekondari Kagera bw. Florian Kimolo ikiwa ni msaada uliotolewa na Airtel kwaajili ya shule za sekondari kanyeranyere, Kirushya na Nyamigogo za Kagera, Hafla ya Makabidhioano imefanyima katika shule ya sekondari kanyeranyere ya wilaya ya Muleba -Kagera.Mwishoni mwa wiki. Airtel imekabidhi Vitabu vyenye thamani ya shilingi milioni 9
Wanafunzi wa shule ya sekondari Kanyeranyere ya wilayani Muleba mkoani Kagera wakiwa wameshikiria vitabu vya sayansi na hisabati walivyokabidhiwa na kampuni ya Airtel mwishoni mwa wiki.Vitabu vilivyokabidhiwa vinathamani ya shilingi milioni 9

* Shule za sekondari za kanyeranyere, Kirushya na Nyamigogo, Kagera zakabithiwa vitabu hivyo 

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kupitia mradi wake wa shule yetu imeendelea kutoa mchango wake katika sekta ya elimu ili kuboresha elimu, kuongeza idadi na ufaulu wa wanafunzi wa sayansi na kupunguza uhaba wa vifaa vya kusomea mashuleni. Airtel imefanya hivyo kwa kutoa msaada wa vitabu vya kufundishia katika shule 3 za sekondari zilizoko Mkoani Kagera mwishoni mwa wiki hii.

Shule zilizofaidika na msaada wa vitabu hivi ni pamoja na shule za sekondari za Kanyeranyere iliyoko muleba, Kirushya wilayani Ngara pamoja na Nyamigogo iliyoko Biharamuro kagera

Akiongea wakati wa halfa fupi ya kukabidhi vitabu vya masomo ya sayansi na hisabati Afisa elimu wa shule za sekondari mkoani Kagera Florian Kimolo alisema" shule nyingi za sekondari katika mkoa wa Kagera zimekuwa na upungufu mkubwa wa vifaa vya kujifunzia na kufundishia sanjari na uhaba wa vifaa vya maabara na walimu. Kutokana na upungufu wa vitendea kazi katika shule mbalimbali za sekondari hapa nchini tunaomba wadau wa elimu kujitokeza katika kusaidia kulitatua tatizo hilo ili shule hizo ziweze kufikia malengo yaliyokusudiwa.

Tunashukuru sana Airtel kwa mchango wao katika elimu na katika kuhakikisha tunapata wanafunzi wengi wa masomo ya sayansi na walimu wanapata vitabu vya kutosha katika kufundishia masomo haya na mwisho kupata ufaulu wa kiwango cha juu.

Naye Meneja mauzo wa Airtel katika mikoa ya Kagera na Kigoma Peter Kimaro alisema " Airtel imejipanga kuendeleza ushirikiano na serikali ili kuisaidia wizara ya elimu kufikia malengo waliojiwekea ikiwemo upatikanaji wa vitabu mashule na kuongeza kiwango cha ufaulu. Hadi sasa kwa kupitia mradi wa " shule yetu tumeweza kufikia shule nyingi za sekondari nchini. Na nimatumaini yetu vitabu tunavyowakabidhi leo vitaleta mabadiliko ya elimu kwa shule hizi na mkoa wa Kagera kwa ujumla.

Naye mkuu wa shule ya sekondari Kanyeranyere iliyoko wilyani Muleba mkoani Kagera alitoa shukurani kwa niaba ya walimu wakuu wa shule za sekondari za kanyeranyere, Kirushya na Nyamigogo na kusema, tunashukuru Airtel kwa kuzikumbuka shule za mkoani Kagera, tunaahidi kuvitumia vizuri vitabu hivi ili kuleta ufanisi zaidi na maendeleo ya
kitaaluma katika shule zetu.

Airtel imekuwa mstari wa mbele katika kuchangia vitabu mashuleni, zaidi ya shule 900 za sekondari hapa nchini zimenufaika kupitia kampeni ya mradi wa kampuni ya simu za mkononi Airtel ujulikanao "Airtel shule yetu".

Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>