Quantcast
Channel: HABARI NA MATUKIO
Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

KUMBE URAFIKI WA WEMA NA KAJALA NI WAKINAFIKI

$
0
0
STAA wa filamu za Kibongo, Kajala Masanja ameibuka na kusema kuwa ushosti wake na Miss Tanzania 2006 /07, Wema Sepetu , uliorudishwa hivi karibuni baada ya kuwekana sawa ni wa kinafiki huku akidai Wema ni kigeugeu.

Staa wa filamu za Kibongo, Kajala Masanja akizungumza kwa kujiamini mbele ya waandishi wetu, juzi Jumatano pande wa Mikocheni jijini Dar es Salaam, Kajala alisema : “Wema ni mnafiki kabisa. Upatanisho wetu ni wa uongo . Mimi moyoni nimeondoa kinyongo lakini mwenzangu naona kama bado ana donge moyoni. ”

Kajala alisema hayo alipoulizwa sababu ya kutoonekana kwenye tukio la futari lililofanyika nyumbani kwa mama mzazi wa Mbongo Fleva , Nasibu Abdul ‘ Diamond ’ , Sanura Kassim ambaye ni mkwe wa shosti wake huyo.

Katika tukio hilo, mama Diamond alifanyiwa sapraizi ya nguvu alipokabidhiwa gari kali aina ya Toyota Lexus Harrier kama zawadi ya bethidei yake, ambayo ilitolewa na meneja wa Diamond , Babu Tale kwa niaba ya mwanamuziki huyo ambaye alikuwa safarini nchini Marekani .

Miss Tanzania 2006 /07, Wema Sepetu, “Tunakubaliana kuwa kitu kimoja lakini mwenzangu anaonekana ana kinyongo. Hebu angalia , anawezaje kuacha kunialika kwenye shughuli muhimu kama ile kama kweli tumepatana ? Mbona amealika watu wengi lakini mimi ameniacha ? Wema aache unafiki bwana.

“Mbaya zaidi , hivi juzi tu ameweka picha ya msichana mmoja anayekaa China, huyu mdada anaitwa Sabrina , niliwahi kugomabana naye , lakini yeye amemuweka Instagram na kumwandikia maneno kibao ya kumsifia akim- wish happy birthday, hapo si kama ananisimanga ? Wema si mkweli, ” alisema Kajala.

Akizungumzia ishu hiyo , siku ya tukio Wema alisema : “Ukiniuliza kuhusu Kajala kutokuwepo hapa, kwa kweli utakuwa kama unanichanganya tu maana leo sijashika simu muda mrefu sana.

“Hata ujio wangu hapa nilikurupushwa , ndiyo maana sijakumbuka kumuita Kajala , lakini tuko vizuri na mara ya mwisho tumeongea jana (Jumapili ) usiku tu , ” alisema Wema . Mdau akifunguka; Yeye ndo mnafiki kipindi anamkosea hakujua aache unafiki kajala alitaka akaribishwe ili iweje tena amuache Wema wetu kabisa wanapenda kumkosea ovyo kwa kuwa walishajua kuwa ana moyo wa huruma, hebu amuache apumue mtoto wa watu kwani yeye alitaka wamalize vipi Wema kaamua kuachana na wewe japo yameisha hataki ukaribu tena na wewe, nani alikwambia bahati huja Mara mbili, mbona Wema huwa  aongei chochote jamani, wewe ndiyo utakuwa unamtafuta Kajala wewe acha unafiki na kuwapa magazeti vya kuongea na kuandika au hujaonekani kwenye magazeti siku nyingi unatafuta kiki kupitia magazeti sio kama ulikuwa na la kusema mngesemezana kimya kimya.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>