Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida, Iddy Mnyampanda akizungumza shule ya sekondari Kinyeto.
Na Hillary Shoo, SINGIDA.
Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini Mkoani Singida, Lazaro Nyalandu ametoa mchango wa mabati 420 yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 10 kwa shule mbili za sekondari za Kata za Mtinko na Kinyeto.
Mchango huo ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi zake kwa wananchi wa Jimbo hilo kuchangia katika ujenzi wa maabara mbalimbali kwenye shule za sekondari za Jimbo hilo.
Akikabidhi msaada huo kwa Niaba ya Nyalandu ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Singida Narumba Hanje aliwataka wananchi kuheshimu michango ya Mbunge wao na kuachana na porojo za siasa za mitaani.
Diwani wa Kata ya Kinyeto, Francisco Ng’eni akizungumza kwenye shule ya sekondari Kinyeto wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya mabati 200.
“Nataka niwaulize swali hivi ni wananchi ndio wenye matatizo au ni sisi viongozi, jibu ni rahisi ni sisi viongozi ndio wenye matatizo, haiwezekani Mbunge anatoa msaada mkubwa namna hii halafu watu wanajipitishapitisha wakitukana.” Alisema Hanje kwa hasira.
Aidha alisema wapo watu wanaompaka matope Waziri Nyalandu, lakini matunda yake yanaonekana na anaendelea kutekeleza ahadi zake.
“Mimi inanishangaza sana kuna watu wameanza kujipitisha pitisha huko na wengine wanatukana kisa eti ni kaligi sijuji Mpombo Cup, fanya vitu vionekane sio maneno maneno kaka, na mimi ndiye mtekelezaji mkuu wa Ilani ya Chama Willaya hii.” Alisema Hanje kwa kujiamini.
Diwani wa Kata ya Kinyeto, Francisco Ng’eni akipokea msaada wa mabati 200 kutoka kwa Mwenyekiti Hanje kwa niaba wa Mbunge wa Jimbo hilo Mhe, Lazaro Nyalandu.
Katibu wa Mbunge Lazaro Nyalandu , Elia Digha, msaidizi wa Mbunge Ellen Mutalemwa wakimsikiliza Mwenyekiti Hanje Kinyeto.
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye viwanja vya shule ya sekondari ya Mtinko.
Mwenyekiti wa CCM Singida vijijini, Narumba Hanje akizungumza na wananchi wa Kata ya Mtinko wakati wa kukabidhi mabati 220.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Singida Vijijini, Narumba Hanje (kulia) akimkabidhi mabati 220 yenye thamani ya shilingi milioni tano Afisa Mtandaji wa Kata ya Mtinko Jimbo la Singida Kaskazini, Eliufoo Mkanga katika hafla fupi iliyofanyika jana katika shule ya Sekondari ya Kata ya Mtinko , mabati hayo yametolewa kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa maabara na Mbunge wa Jimbo hilo Mhe,Lazaro Nyalandu.
Hili ni jengo la maabara ya sekondari ya Kinyeto likiwa katika hatua ya lenta.
Kibao kikionesha shule ya sekondari Mtinko.(PICHA ZOTE NA HILLARY SHOO).