Wanaohusika na ubadhirifu wa fedha za manunuzi ya Umma watangazwe hadharani ili wafahamike na kuchukuliwa hatua stahil kwani wamekuwa wakitumia fedha za umma kwa manufaa yao bila ya kujali.
Changamoto hiyo ilitolewa na waziri wa fedha Saada Mkuya Salum wakati akifungua warsha ya ppra kuhusu sheria ya ununuzi wa umma kwa wakurugenzi wa bodi,wakuu wa taasisi na mashirika ya umma na wakala wa serikali jijini.
Mkuya alisema kumekuwepo na malalamiko mengi katika manunuzi ya umma huku akifafanua kuwa takwimu zinaonyesha asilimia sabini ya bajeti ya kawaida na asilimia mia moja ya bajeti ya maendeleo hutumika kufanya ununuzi kiwango ambocho ni kikubwa sana hivyo ni muhimu kuweka udhibiti wa ununuzi wa sekta hiyo.
Waziri alisema upotevu au ubadhilifu unaoweza kujitokeza unaweza kuliingizia taifa hasara kubwa kwani imeonekana asilimia kumi na tano hadi ishirini la pato la taifa kutumika katika manunuzi ambapo kiwango hichi ni kikubwa sana.
‘’Nawakumbusha kuwa sekta ya manunuzi ya umma imekuwa ikiliingiza taifa kwenye deni kubwa hivyo mnawajibu mkubwa wa kudhibiti manunuzi ili kuipunguzia serekali mzigo kwani bila ya kufanya manunuzi yenye kukidhi kwa wakati mtakuwa hamkuisaidia serekali bali mtakuwa mmefanya hiyana” alisema Mkuya.
Kwa upande wake mwenyekiti wa bodi ya ppra balozi dkt matern lumbanga amesema warisha imeandaliwa kwaajili ya kuwaelimisha walengwa kuhusu sheria ya ununuzi wa umma ya mwaka 2011 na kanuni zake za mwaka 2013 lengo likiwa ni kuboresha ununuzi wa umma
Lumbanga alisema kuwa Tanzania imekuwa ikipoteza fedha nyingi kwenye manunuzi ya umma hivyo mnao wajibu wa kukabiliana na changamoto hiyo huku akitanabaisha kuwa ripoti ya utendaji wa ppra ya mwaka wa fedha 2012/13 imebainisha kwamba zaidi ya trillion nne zilitumiwa na taasisi za umma 265 kufanya manunuzi ya ukandarasi wa ujenzi ikiwemo vifaa na huduma.
Huku akisema kuwa maboresho yataendelea kuwepo kwenye sekta ya manunuzi ilikuendana na viwango na sheria mpya ya manunuzi ya mwaka 2011 huku akiwasihi wadau na wazabuni kufuata matakwa ya shria hiyo pia kuomba ushauri badala ya kukimbilia kwenye vyombo vya habari kutoa malalamiko.