Baadhi ya mabondia Makocha pamoja na wadau wa mchezo wa ngumi wakiungana pamoja wakati wa msiba wa bondia Sadat Miyeyusho aliezikwa leo katika makaburi ya FM Kinondoni Dar es salaam picha na www.superdboxingcoach. |
Bondia wa siku nyingi Koba Kimanga akiwa amemeba jeneza lenye mwili wa marehemu Sadat Miyeyusho kwenda kuzika katika makaruri ya FM Kinondoni Dar es salaam picha na www.superdboxingcoach. blogspot.com
Mabondia Nassibu Ramadhani na Fransic Miyeyusho wakiwa katika msiba wa bondia mwenzao Sadat Miyeyusho picha na www.superdboxingcoach. blogspot.com
Kocha wa Ngumi Cristopher Mzazi akiwa kabebwa kwenye poikipiki tayali kwenda kuzika
Mamia ya waombelezaji wakiupereka mwili wa marehemu Sadat Miyeyusho kuzika
Baadhi ya waombelezaji wakiwa na jeneza lenye mwili wa marehemu Sadat Miyeyusho kwa ajili ya kupereka makaburi ya FM Kinondoni kuzika picha na www.superdboxingcoach. blogspot.com
Waombelezaji wakiwa wanazika mwili wa marehemu Sadat Miyeyusho katika makaburi ya FM Kinondoni
Baadhi ya waombelezaji wakiwa makaburini picha na www.superdboxingcoach. blogspot.com
Na Mwandishi Wetu
MAMIA ya wakazi wa jiji la Dar es salaam wamejitokeza katika maziko ya bondia Sadat Miyeyusho yaliyofanyika katika makaburi ya FM Kinondoni Dar es salaam bondia huyo aliefariki kwa ajali ya pikipiki juzi amezikwa jana katika makaburi hayo ya Kinondoni
Historia fupi ya marehemu inaonesha kuwa alianza ngumi mwaka 2006 ambapo mpambano wake wa kwanza katika ulimwengu wa masumbwi kacheza na Adam Yahya na kushinda kwa point mpambao uliofanyika katika ukumbi wa DDC Mlimani Park mpambano wake wa mwisho katika maisha yake ya mchezo wa ngumi ni mwaka 2012 alipopambana na Issa Nampekecha katika ukumbi wa Friends Corner Hall na kupoteza kwa point bondia huyo ameshacheza na mabondia wanaotamba kwa sasa kama Ramadhani Shauli na Juma Fundi ambao alisha wai kuoneshana nao umwamba katika uringo.
Bondia huyo ameacha mke na watoto mungu awape subra familia ya marehemu pamoja wa wafiwa wote katika kipindi hiki cha msiba wa mpendwa wetu Sadat Miyeyusho mbele yake nyuma yetu.