Quantcast
Channel: HABARI NA MATUKIO
Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

NANI NI NANI LEO????? BRAZIL NA UJERUMANI

$
0
0
Timu ya Brazil.

Na Mwandishi Wetu, Belo Horizonte, Brazil. 

Ujerumani inakutana na Brazil inayocheza kwa nguvu nyingi katika mchezo wa nusu fainali ya kwanza ya Kombe la Dunia, huku wenyeji hao wakipania kutwaa ubingwa kama zawadi kwa Neymar.

Kikosi cha kocha Joachim Loew, Ujerumani inahitaji kufikia mafanikio ya 2002, ilipofanikiwa kucheza fainali dhidi ya Brazil licha ya kuchapwa mabao 2-0, na sasa itakuwa katika mchezo utakaopigwa mjini Belo Horizonte.

Brazil inalazimishwa kucheza kwa nguvu ikiwa bila mchezeshaji wao, Neymar aliyeumia na nahodha wao, Thiago Silva mwenye kadi mbili za njano, wakisaka nafasi ya kutwaa taji hilo nyumbani katika Uwanja wa Maracana, Jumapili.

Taifa zima limeumizwa na kukosekana kwa Neymar mwenye miaka 22, ambaye aliumia uti wa mgongo katika mchezo wa robo fainali dhidi ya Colombia, lakini Ujerumani inatamani kama nyota huyo angekuwapo.
Timu ya Ujerumani.

“Siku zote inakuwa vizuri kama wapinzani wenu wametimia, lakini hilo pia litaifanya Brazil iwe pamoja na watataka kushinda kwa ajili yake (Neymar),” alisema kiungo wa Ujerumani, Bastian Schweinsteiger.

Brazil walimchezea vibaya kiungo wa Colombia, James Rodriguez, wakati Colombia walipokutana na Brazil kabla ya Juan Zuniga kumgonga Neymar, tukio lilimfanya nyota huyo wa Selecao kupelekwa haraka hospitali.

“Neymar ametufanya tuimarike. Ana uwezo wa kuuamua mchezo wowote, hivyo kucheza bila yeye itakuwa ngumu,” alisema Willian, winga wa Brazil.

“Tunajua ubora tulionao. Sote tuna huzuni ya kumpoteza, lakini kwa sasa tuna nguvu zaidi kutokana na kile kilichotokea na tuko tayari kutimiza ndoto zetu.”

Nyota huyo wa Chelsea mwenye miaka 25, Willian au Bernard wanapewa nafasi ya kuanza katika nafasi ya Neymar wakati watakapoivaa Ujerumani hii leo.

Schweinsteiger aliugusia mchezo huo akisema mwamuzi anatakiwa kuwa makini zaidi juu ya mchezo wa Brazil, ambao wamecheza faulo 59 katika michezo miwili iliyopita, ukilinganisha na 29 za Ujerumani katika michezo kama hiyo.

“Wabrazili kwa sasa si wachawi wa soka kama walivyokuwa zamani, timu yao imebadilika sana na hata aina yao ya uchezaji,” alisema Schweinsteiger.

“Rafu nzito kwa sasa ni sehemu ya soka yao, ni jambo ambalo tunatakiwa kuwa nalo makini mno uwanjani, pia kwa mwamuzi,” aliongeza.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>