Quantcast
Channel: HABARI NA MATUKIO
Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

WADAU WASEMAVYO KUHUSU SAKATA LA FLORA MBASHA NA MUMEWE

$
0
0
Pichani ni Flora Mbasha kulia akiwa na Masanja Mkandamizaji wakiimba neno la bwana.

Na Kambi Mbwana

"Tusamehe dhambi zetu KAMA SISI TUNAVYOWASAMEHE WALIOTUKOSEA" ... Pichani ni mwanadada Bi. Flora Mbasha akiendelea kumtumikia Mungu kwa nyimbo za Injili jijini Mwanza. Hii hainifanyi nisiendelee kumfikiria yeye na sakata la mumewe hadi kutajwa kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na Mchungaji Gwajima. Kusema ukweli nawaza sana! Nawaza namna muziki wa injili unavyoheshimika na haya yanayosemwa sasa. Ndio inawezekana kuna makosa makubwa yamefanywa aidha kwa Mbasha au kwa Flora. Lakini kusamehe si kupo? Au wenzetu hawajui msamiati huo? Na hasa Flora ndio hataki kumsamehe mumewe wake, wakati anajua neno la Mungu linavyosema na kuhitaji. Basi kama ndio hivyo, namshauri dada Flora aache kutumia jina la Flora Mbasha maana Mbasha mwenyewe si hamtaki kiasi cha kufurahia alipoburuzwa kortini? Sioni maana ya kumpinga kondoo eti mchafu wakati mchuzi wake unakunywa na chapati... Dunia hii!!!.

Damas Damian Kawonga: Kambi Mbwana hata mimi najikuta nikimuonea huruma sana Bw. Emmanuel Mbasha, pia najikuta namchukia sana Flora baada ya Sakata hili. Lakini nikitafakari sana, huenda wakati mwingine hatumtendei haki Flora, tusubiri uamuzi wa mahakama kabla ya kumhukumu Flora, hatujui nini kilikuwepo ndani ya nyumba yao.

Kimaro V Icky: Kambi Mbwana tatizo mnaishi kwa kukariri, na pia sio kosa lako kwasababu vyombo vya habari vimekuwa vikiripoti upande mmoja tu wa mbasha, flora mwenyewe ajafunguka kwa undani sakata lake, si ajabu kiatu chake ukipewa wewe hakikutoshi, achene kumuhukumu Flora, mpaka ameamua kutoka hujui kilichopo nyuma ya pazia, na msimuangalie tu mbasha, vipi kuhusu huyo anayedaiwa kubakwa? mbona hamumuonei huruma, anyway, mwisho wa siku tuwaachie wenyewe matatizo yao na mahakama ndio itakayoamua, si mimi wala wewe anayejua kilichopo nyuma ya pazia.

Makamba Musa: Mnh' langu sikio tu.

Kambi Mbwana: Dada yangu Kimaro V Icky, sijahukumu kabisa! Nimejikita kwenye msamaha kama neno la bwana linavyoagiza. Hao wawili watakuwa wamekoseana sawa, ila kusamehe si kupo? Ukizingatia kuwa wanaishi kwa kumtumainia Mungu kwa injili. Kusema ukweli kabisa, hata dada Flora anakosea tena sana. Yeye ni tofauti na akina Ray C, Dayna Nyange wanaoimba muziki wa kidunia. Yeye anapaswa kuwa mfano wa kuigwa. Sitaki kuzama sana kwenye sheria, maana mara zote inaweza kutoa haki! Tuwaangalie akina Flora kama vioo vya jamii juu ya Injili na neno la Mungu.

Classic Rabia: Sisi wanawake ni wavumilivu na wasamahevu mnoo. Lakini ukimuona mwanamke kuondoka kwa mumewe au mpenzi waliyekuwa wakiishi kwa shida na raha, ipo namna. Kwa kweli wakati mwingine nasimama upande wa Flora Mbasha, sidhani kama ni mjinga kiasi gani ashindwe kusamehe, lakini huenda aliyofanyiwa na huyo mwanaume ni makubwa!! Mimi katika sakata hili nimejifunza kitu, kwamba mwanaume ni mswahili aliyeshindikana, ambaye hana kabisa kifua cha uanaume, aliyeshindwa kusimama kwa ajili ya ndoa yake badala yake ameivunja kwa mikono yake. Huwezi kumpaka kinyesi mkeo na baadaye hurudi kumtaka akusamehe!!! Kaka Kambi Mbwana, acha kabisa aisee... kuna wakati inatakiwa tufike tuache mambo kama yalivyo kwani mjuaji ni Mungu pekee.

Prisca Malekela: Huwezi kuimba neno la bwana Kambi Mbwana.

Classic Rabia: Mmejuaje kama hajamsehe?? Au msamaha ni lazima wawe pamoja tena??! Je mnaelewa mazingira waliyokuwa wakiishi... Mungu ana makusudi kwa kila kitu. Kama ni Flora ama ni Mbasha basi nadhan kila mmoja atahukumiwa kwa kile anachostahili, lakini si hukumu zetu sisi binadamu.

Kambi Mbwana: Dada yangu Classic Rabia, mpendwa wangu, natambua uvumilivu huo mliokuwa nao wanawake! Lakini nilichogundua sasa jinsia mbili zinavutia kwake! Wanawake mpo upande wa Flora na wanaume tupo upande wa Mbasha! Tutoke huko. Tusimame kwenye haki na si sheria kama alivyosema kaka Damas hapo juu. Hii ni kwasababu, tukisimama kwenye haki, basi tutajua namna gani hawa wenzetu wanatakiwa kusameheana ili maisha yaendelee! Yanayosemwa upande wa Flora ni ma big na tunayosikia kutoka kwa Mbasha hali kadharika. Tunasema Mbasha amebaka au anatembea na shemeji yake! Sawa, je ndio malipo ya kuanzisha uhusiano na mchungaji! Tena uhusiano wa kimapenzi. Wakati sakata hili linaibukia, nilikuwa makini kusikiliza hoja za Flora, badala yake sijasikia zaidi ya kuelekea mahakamani ambapo sasa si ruhusa kuzungumzia mambo yaliyopo mahakamani. Narudia tena, unawezaje kuimba neno la Mungu, kuhamasisha watu wamche Mungu wakati mwenyewe hujamrudia Mungu? Am sorry kwa hili, ila mnaomuweza huyu dada mwambieni atulize kichwa chake atetee ndoa yake na si kuhangaikia kuivunja coz kwa dini yao, hata kama wakitengana sidhani kama anaweza kuolewa tena!

Raymond Minja: da prisca flora kanukuliwa mara kadha na vyombo vya habari na alikata mara tano kuwa hataki ndoa sasa Mungu gani anayemuabudu mnafiki mkubwe huyu asiye na chembe hata ya aibu kaokotwa huko kafikia mafanikio anaona aliyemtoa hana maana anakimbila kwa wenye hela hizo hela zitamtokea puani siku ya mwisho.

Kambi Mbwana: Dada prisca Malekela, sijakusoma! Fafanua hoja yako! Nani hawezi kuimba neno la bwana! Mimi au? Tehe tehe teheeee!

Kambi Mbwana: Dada yangu Classic Rabia, Flora hataki kabisa kusikia mtu anayeitwa Mbasha! Ndio maana nasema hajamsamehe! Hivi, kwa mfano wametengana sasa, Flora anaweza kuolewa tena? Mbasha anaweza kuoa tena? Aha ha ha haaa! Kwa hiyo wanataka kuvunja ndoa yao ili waendeleze libeneke nje ya uwanja? Aha ha ha ha ha haaaaa. Mungu okoa hiki kizazi cha snakeeeeeeeee...

Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>