Mathias Rugaimukamu
ANGALIA SAFARI YANGU YA ELIMU NA KWANINI NASEMA NI KWA NEEMA TU.
Nilianza chekechea 1994 pale Rwambaizi na kuchaguliwa km wasioweza kusoma na kuandika lakin umri umezid na kupewa nafasi darasa la kwanza km residue i.e makapi (mabaki). Nikamaliza la kwanza nikiwa wa mwisho, nikaingia la 2 bila hata kujua kusoma na kuandika bado nilizidi kuwa wa mwisho mpaka muhula wa pili Dec 1997, nikawa mtu wa 4 katika darasa la wabovu. Baadae tukaunganishwa na wale wajivuni (wakali) kuingia la 3 hapo ndo nikaanza kuona kama naweza kwani muhula wa 1 nikawa wa 12 na kumaliza wa 5 katika mtihani wa kuingia la 4.
Mwaka 1994 ikawa ni mara yangu ya kwanza kuwa mtu wa kwanza nikiwa darasa la 4 sikuwahi kutoka pale mpaka darasa la 6 baada ya hali ya maisha kuwa magumu na kuamua kuacha shule. Nakumbuka walimu waliweka vitisho na kuanza kunitafuta hatimaye nikarudi na kufanya mtihani nikawa wa 8.
Nililia sana kwenye mtihani huo wa mwezi wa 9 nakumbuka kwa wanaoijua shule ya msingi Rwambaizi ilikuwa kwenye lile darasa la pembeni ya staff ambalo halikuwa na sakafu. Nikarudi darasani na kuanza kusoma mara baada ya msamalia mwema MWL. PONSIAN MZARE kunichukua nikaishi kwake.
Nikaanza kuirudia nafasi yangu ya kwanza mpaka namaliza darasa la 7 nakumbuka sana mwalimu Jumbe alikuwa msaada mkubwa kwangu kaika lugha kwani ilikuwa inanisumbua japo nilikuwa mtundu sana. Nakumbuka siku moja alinilisha maganda ya mihogo kwa utundu wangu.
Baada ya kumaliza la darasa la 7 nikachaguliwa kwenda shule ya vipaji maalumu mkoani Mwanza inaitwa BWIRU BOYS. Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Rwambaizi Bw. C. Mlenda ... aliniita na kunishauri nisomee nyumbani kwani alijua sana uwezo wa familia yetu. Nilisita sana japo nikaja kukubaliana naye baada ya kuwa napenda sana michezo ambayo ilikuwepo pale shuleni nikadhani sitoikuta Bwiru.
Nilijiunga na shule ya sekondari mwaka Bwiru Boys mwaka 2003 mwezi wa 3 wakati wenzangu walitangulia mwezi wa kwanza. Nikakuta wamefika mbali kwani Bwiru Boys ya kipindi hicho ilikuwa hatari sana katika kufundisha. Kaka yangu Mathias ambaye tulisoma wote Mwenge ndiye nilikuwa natumia sana madaftari yake akirudi toka shule hapo mimi bado nikiwa nyumbani.
Tukafanya mtihani wa mwezi wa 3 nikawa na wastani wa 84 na kutangazwa kuwa mtu wa 1. Nilipata misukosuko sana kwani hawakuamini kutokana kwamba nilichelewa, hivyo walijua kwamba natazamia.
Tulipofanya tena mtihani wa mwezi wa 6 nikawa wa 1 pia, mwezi wa 9 hivyo hivyo wa 1 ila tulipofanya mtohani wa mwezi wa 12 nikawa mtu wa 2. Nakumbuka mlenda alinizomea sana kuwa nimekuja nikiwa mkali sasa naanza kushuka, wa kwanza alikuwa Mwenzangu Cyprian. Nilipenda sana kujisomea japo nyumbani walipenda kutupeleka shambani RWENJUBU kwa wale wa wazaliwa wa Bukoba mtakuwa mnapajua.
Ilipofika kidato cha Pili, kwangu ulikuwa mzuri sana kwani nilikuwa nimejinoa vyema upande wa kufundishwa na kujisomea, ulipofikia mtihani wa Mock nikawa mtu wa 2 Kiwilaya (Karagwe) mwaka 2004 na kila somo nikiwa katika kumi bora. Nikaendeleza kukazana mpaka ilipofika mtihani wa taifa (NECTA) nikawa na wastani wa 72. Mambo hayakuwa mazuri kwani nilitaka niwe kwenye top ten kitaifa.
Kuingia kidato cha tatu nikazidi kuwa vizuri kwani nakumbuka mwaka huo 2005 niliweka rekodi ya kuwa na wastani wa 92. Nilifurahi sana na kujipa moyo kuwa nitayatengeneza maisha yangu niliyajenga kwenye mpira na masomo. Sikuwa hata mpenzi japo nilikuwa karibu sana na rafiki yangu mkubwa Elvida Gregory tangia form 1 na watu wakidhani tulikuwa wapenzi ... masikini nilikuwa kadogo sana.
Nilicheza sana mpira na kupenda mziki kwani nilikuwa mtu wa kujichanganya pale ninapokuwa nahitajika sikupenda kuwa book worm.
Tukiwa kidato cha nne nikajiwekea malengo na hatimaye kwenye Mock nikawa na DIV 1 point 13 na kuwa mtu wa kwanza Kiwilaya ila wa 15 Kimkoa Kagera. Nikamshukuru Mungu aliyezidi kunibariki mpaka nafanya mtihani wa taifa wa kumaliza kidato cha nne (NECTA) mwaka 2006 nilikuwa mgonjwa ila nilifanikiwa kupata DIV 1 ya point 13 nikiwa nimekaa sawa katika masomo ya Sayansi na Arts na nilipenda sana somo la Historia kwa sababu ya mwalimu Frida Kitale.
Nikachaguliwa SHINYANGA SEC SCHOOL kwenda kusoma PCM watu wakaniambia na kunizomea kwanini nimechagua shule mbovu, nikasema Mungu nisaidie. Nikiwa nasubiria nafasi ya shule nikawa najitolea kufundisha shule ya sekondari Nyakahanga kusudi nipate vihela vya kwendea shule.
Mnamo tarehe 01/04/2007 nikajiunga rasmi na shule ya Sekondari Shinyanga huku nikiwa sijasoma kitu chochote nikaanza kukazana, nikaandika notes na kuanza kujisomea kwa kufundishwa na wenzangu. sikuwahi kwenda tution kwasababu uwezo ulikuwa mdogo sana. Nikiwa pale nikapata rafiki yangu ambaye mpaka sasa ni kama ndugu yangu Bw. NICODEMAS BALAMA ambaye sasa anasomea upadri baada ya kuhitimu shahada yake ya Information System pale Chuo Kikuu Dodoma (UDOM).
Tuliishi na kusoma vizuri mpaka namaliza mwaka 2009 mwezi wa pili nikiwa kidedea kwa DIV 1 ya point 4. Sikuweza kuomba chuo mwaka huo licha ya jitihada za Prof. Kamuzora kutaka niende kwani nilipaswa kufanya kila kitu kuakikisha na ndugu yangu anaenda shule. Nikaanza kujitolea pale Nyakahanga 2009 mwezi wa 3 mpaka wa 5 na kuhamia Rwambaizi ambapo nimekaa mpaka 2010 mwezi wa 1 na akina Ditrick, Sweetbert, Joronimo, Edmackius na wengine wengi na baadae kwenda shule ya sekondari Kaisho mwaka 2010 ambapo nimefundisha mpaka nakuja chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwezi wa 10 kuchukua jiwe langu katika Bsc in Telecommunication Engineering.
Tukiwa chuo umasikini jamani ni hatari kwani unachangia sana kumnyima mtoto wa maskini ufauru ila licha ya misukosuko yote nimefanikiwa kuhitimu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) tarehe 04/07/2014 ni safari yangu hiyo ambayo nimepita japo mengine ni siri binafsi, Mungu ni mkuu kwani kwa mtu wa aina yangu usingetegemea afike hapa.
ASANTE SANA MAMA KUSIMAMA KIUME MPAKA SASA SINA CHA KUKULIPA. Mwenyezi MUNGU TU NDIYO ANAJUA.