Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya ORIFLAME katika upande wa Afrika ya Mashariki bwana Klas Kronaas akifanya uzinduzi rasmi kwa kufungua bango lililokuwa linaonesha bidhaa zao mpya.
Mkuu wa masoko wa kampuni ya Vipodozi ya ORIFLAME, Harry Nyagi akizungumza jambo kwenye sherehe ya uzindizi wa bidhaa mpya za kampuni ya ORIFLAME
Mwonekano wa bidhaa zilizozinduliwa na kampuni ya ORIFLAME nchini Tanzania.
Fortunata Nkya akizungumza na waandishi wa habari kwenye sherehe ya utambulisho wa bidhaa za ORIFLAME katika soko la Tanzania.
Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya ORIFLAME katika upande wa Afrika ya Mashariki bwana Klas Kronaas akielezea namna bidhaa zao zinavyotengenezwa kwenye kwenye sherehe ya utambulisho wa bidhaa zao katika soko la Tanzania.
Bi. Maznat Yusuph Sinare akieleza namna bidhaa na vipodozi mbalimbali vilivyokuwa na ubora wa kimataifa kwenye uzinduzi wa vipodozi vipya vya kampuni ya ORIFLAME.
Wageni walioalikwa kushuhudia uzinduzi huo wakijadiliana jambo kuhusiana na Bidhaa za kampuni ya ORIFLAME.
Baadhi ya wadau waliofika kwenye uzinduzi huo wakifuatilia kwa makini maelekezo ya bidhaa za kampuni ya ORIFLAME.
Kampuni ya Vipozi vya aina mbalimbali vya urembo OriFlame wamefanya maonesho ya Bidhaa zao Tarehe 2.07.2014 katika ukumbi wa Zanzibar katika Hotel ya Hyatt Regency (The Kilimanjaro Hotel).
Kampuni hiyo yenye wigo mpana wa kibiashara ambayo ina matawi zaidi ya nchi 20 duniani na pia Katika Mabara manne ya Duniani wametambulisha bidhaa zao mpya kwenye soko la Tanzania ambazo ni marashi ya kike na kiume pamoja na vipodozi mbalimbali,
Juu Pichani ni Maznat Yusuph Sinare kutoka saloon ya Maznat Bridal mtaalamu wa kuchanganya Vipodozi akimremba mwanadada Janeci Maluli ili kuonyesha aina tofauti za vipodozi vya Kampuni hiyo.
Maza Yusuph Sinare akimpaka wanja wa nyusi Mwanamitindo Janeci Maluli kwenye sherehe za uzinduzi wa bidhaa mpya za kampuni ya ORIFLAME iliyofanyika kwenye ukumbi wa Zanzibar katika Hotel ya Hyatt Regency (The Kilimanjaro Hotel).