Meneja Mauzo wa Kampuni ya Bia Mkoa wa Mbeya Vivianus Rwezaura akikabidhi kombe kwa nahodha wa timu ya Green City, Issa Nelson baada ya timu hiyo kuibuka mabingwa wa Castle Lager Perfect Six Kanda ya Kusini.
Mashindano ya Castle Lager Perfect Six ngazi ya fainali za Kanda yamefikia tamati kwa kishindo baada ya timu ya Green City ya Jijini Mbeya kufanikiwa kutwaa ubingwa wa Castle Lager Perfect Six baada ya kuichabanga Timu ya Savannah kutoka Mkoani Iringa kwa mabao 8-3.
Michuano hiyo ambayo ilichezwa katika Viwanja vya City Pub, jijini Mbeya ulikuwa ni wa vuta nikuvute huku kila upande ukitaka kuchukua ubingwa wa kanda hiyo kuungana na kanda zingine saba Jijini Dar es salaam katika fainali ambazo zitawapatia washindi fursa ya kwenda kutembelea uwanja wa Camp Nou kushuhudia mechi za FC Barcelona na kutembelea maeneo mbalimbali ya jiji la Barcelona.
Kanda ya kusini ndio imekamilisha mchakato wa kupata wawakilishi wa kanda ambazo zitashiriki kwenye fainali za taifa zitakazochezwa mwezi Agosti jijini Dar es salaam.
Kanda ya kusini ndio imekamilisha mchakato wa kupata wawakilishi wa kanda ambazo zitashiriki kwenye fainali za taifa zitakazochezwa mwezi Agosti jijini Dar es salaam.
Mchezo huo ulihusisha timu nne kutoka mikoa ya Nyanda za Juu Kusini.
Timu zilizoshiriki katika mchuano huo ni Green City na White Stars kutoka Jijini Mbeya,Savannah na Gaddafi kutoka Manispaa ya Iringa.
Green City ilifanikiwa kuingia katika hatua hiyo baada ya kuifunga timu ya Gaddafi mabao 9-0 wakati washindi wa pili Savannah ilifanikiwa kuingia fainali kwa kuifunga timu ya White Star ya Mbeya mabao 5-3.
Green City ilifanikiwa kuingia katika hatua hiyo baada ya kuifunga timu ya Gaddafi mabao 9-0 wakati washindi wa pili Savannah ilifanikiwa kuingia fainali kwa kuifunga timu ya White Star ya Mbeya mabao 5-3.
Katika mchezo huo wa fainali magoli ya Green City yalifungwa na Issa Nelson aliyefunga magoli 3 Castro Litongwale aliyefunga magoli 3 na Lambert Lameck aliyefunga magoli 2.
Magoli ya Savannah yalifungwa na Enhard Mgeni magoli 2 na Johnson Ngogo Aliyefunga bao 1.
Akizungumza kabla ya kukabidhi zawadi kwa mshindi Meneja mauzo wa bia ya Castle Lager Nyanda za Juu Kusini Vivianus Rwezaura alisema kuwa atatoa ushirikiano wa hali na mali kwa washindi ili wafanikiwe kuwa mabingwa wa Castle Lager Perfect 6.
Naye Meneja wa Bia ya Castle Lager Kabula Nshimo alisema kuwa mashindano hayo yameleta changamoto kwa washiriki na kwamba ana imani ushiriki wa timu hizo umeongeza ari kwa vijana kupenda soka.