Mashabiki wa Timu ya Brazil wakifuatilia mechi kati ya Chile na Brazil. Ambapo Brazil imeibuka kidedea kwa penalti bao 3-2.
Wachezaji wa Brazil wakishangilia baada ya kushinda kwa penalti 3-2 dhidi ya Chile.
Mashabiki Brazil wakishangiia baada ya kutinga robo fainali.
WENYEJI Brazil wameitoa Chile kwa penalti 3-2 katika mchezo wa hatua ya 16 Bora Kombe la Dunia mjini Uwanja wa Belo Horizonte, kufuatia sare ya 1-1 ndani ya dakika 120.
Shujaa wa Brazil alikuwa ni kipa Julio Cesar aliyeokoa penalti mbili za Alexis Sanchez na Mauricio Pinilla wakati Gonzalo Jara aligongesha mwamba, huku Marcelo Diaz na Charles Aranguiz wakifunga.
Penalti za Brazil zilifungwa na David Luiz, Marcelo na Neymar, wakati Hulk na Willian misses walikosa.
Brazil: Julio Cesar, Dani Alves, Thiago Silva, Luiz, Marcelo, Fernandinho, Gustavo, Hulk, Oscar, Neymar, Fred.
Subs: Jefferson, Paulinho, Dante, Maxwell, Henrique, Ramires, Hernanes, Willian, Bernard, Jo, Maicon, Victor.
Chile: Bravo, Mena, Isla, Silva, Alexis, Vidal, Vargas, Medel, Jara, Aranguiz, Diaz.
Subs: Toselli, Albornoz, Carmona, Pinilla, Valdivia, Rojas, Orellana, Beausejour, Gutierrez, Fuenzalida, Paredes, Herrera.
Referee: Howard Webb (England)