MNYANGE atakayefanikiwa kuibuka mrembo wa kitongoji cha Sinza‘Redds Miss Sinza 2014’ katika shindano litakalofanyika leo Ijumaa kwenye Ukumbi wa Meeda Night Club uliopo Sinza jijini Dar es Salaam atazawadiwa kitita cha Sh. 300,000.
Akizungumza jana jijini, Mratibu wa shindano hilo, Tinna Makutika, alisema kuwa mshindi wa pili atajinyakulia Sh. 200,000, mshindi wa tatu Sh. 100,000 huku warembo wengine waliobakia kila mmoja ataambulia zawadi ya kifuta jasho ya Sh. 50,000.
Mratibu washindano hilo alisema kuwa maandalizi ya kinyang’anyiro hicho yamekamilika naanaamini Sinza mwaka huuitafanikiwa kutwaataji la taifa ambalo linashikiliwa na mrembo kutoka Dodoma.
Alisema kuwa warembo wake wamejiandaa kuonyesha ushindani na kila mmoja amejipanga kufanya vizuri ilikushinda taji la Sinza usiku wa leo.
"Mwaka huu nina warembo wazuri na wenye vigezo vyote, naamini mwaka huu nitarudisha heshima ya watu wa Sinza ya kufanikiwa kutoa mshindi wa taji la Redd's Miss Kinondo nina Redd's Miss Tanzania mwaka 2014”, alisemaTinna.
Aliongeza kuwa wamejipanga kuendeleza mazuri ya liyofanywa na Brigitte Alfred, ambaye alitwaa taji la taifa na kupata nafasi ya kuitangaza nchi kwenye mashindano ya dunia ya Miss World.
Alisema pia shindano hilo linatarajiwa kuwa na burudani mbalimbali ikiwamo bendi mahiri ya muziki wa dansi, FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’ ambao wanatamba na Chuki ya Nini.
Kiingilio cha juu katika shindano hilo ni Sh. 10,000 kwa viti maalum na vya kawaida ni Sh. 5,000.
Aliwataja warembo 12 watakaochuana ni Liliani Sandi, Priscar Sarakikya, Agnes Mwikombe, EstaWilson, Rose Lucas, Zubeda Saburi, Tuku Harison, Dorine Benne, Farida Iddy, Qeen latifa Hashim, Jane Masawena Wahida Ahmed.