Quantcast
Channel: HABARI NA MATUKIO
Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

MWANAFUNZI WA IFM ALIYEZAMA BAHARINI APATIKANA AKIWA AMEKUFA, AZIKWA JIJINI DAR

$
0
0
TANZIA

Mkuu wa Chuo Cha Usimamizi wa Fedha IFM, Anasikitika kutangaza Kifo cha Mwanafunzi Abdul-Aziz Mukasa (pichani) mwenye namba ya usajili BIRM/12/71893 kilichotokea tar. 28.1.2013 kwa kuzama baharini. Mazishi yamefanyika tar 30.1.2013 katika makaburi ya Vijibweni.

Hiyo ndiyo taarifa iliyotoka kwa Mkuu wa Chuo cha IFM kuwapa habari wanafunzi wenzake na marehemu.

Mwanafunzi huyo mauti yalimkuta baada ya mezama na kupotelea baharini alipokuwa katika Pantoni akivuka akielekea Kigamboni jijini Dar es Salaam.

TUKIO LENYEWE LILIKUWA HIVI:

Wakizungumza na Kajunason Blog mashuhuda wa tukio hilo, walisema kuwa mwanafunzi huyo alikuwa akivuka na wenzake jioni ya leo kuelekea Kigamboni jijini Dar mara baada ya kutoka kwenye mtihani wake ndipo alipokutwa na mauti hapo.

Sakata hilo lilianza mara baada tu ya Pantoni hilo kukaribia eneo la kivuko cha Kigamboni ndipo mwanafunzi huyo alipoanza kubishano na wanafunzi wenzake kuwa anauwezo wa kuzamia na kupiga mbizi, katika kuwahakikishia hilo alivua viatu pamoja na shati lake na kuwapatia wenzake na kujitosa kwenye maji ili apige mbizi kuwahakikishia wenzake uhodari wake.

"Kiukweli ni jambo la kushangaza sana, ulitokea ubishani wa wanafunzi baada ya mwenzetu huyu kuwa anajisifia kuwa anajua kupiga mbizi ndipo alipovua viatu na shati na kujitosa kwenye maji, kwa bahati mbaya aliangukia upande wa Pantoni lilipokuwa likipiga makasia na kwa kawaida sehemu hiyo maji huwa yanakasi sana hivyo yalimsababishia mwanafunzi huyo kushindwa kuibuka na kumfanya azame katika kina kirefu,"

Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>