WASHINDI wa Chemsha Bongo ya Brazil ambayo inadhaminiwa na Azam TV, Allen John Muhuma na Said Mohammed Muba, wamekabidhiwa zawadi zao leo kwenye ofisi za Global Publishers, Bamaga-Mwenge, Dar.
Washindi hao ambao walifanikiwa kujibu ipasavyo maswali kwenye swali la Chemsha Bongo lililokuwa kwenye magazeti ya Championi ya wiki iliyopita, wamejishidia TV, dekoda ya Azam na dishi.
Wakizungumza mara baada ya kukabidhiwa zawadi zao walisema kuwa hii ni faraja kubwa sana kwao kwa kuwa wameweza kuboreshewa maisha yao na Championi.
“Ukweli hii ni faraja kubwa sana kwangu na familia yangu, nimejisikia vizuri sana na kamwe sitaacha kushiriki kwenye kila toleo,” alisema Muba.
Kwa upande wake Muhuma, alisema awali aliamini kuwa kuna watu huwa wanaandaliwa kwa ajili ya kushinda zawadi hizi.
“Hili limenifanya niamini kuwa Chemsha Bongo hizi ni za kweli, nimefarijika sana na niahidi kuwa nitashiriki kila siku na naamini nitashinda tena.”
Ukitaka kushiriki Chemsha Bongo hii jibu swali ambalo lipo kwenye gazeti la Championi kisha tuma jibu lako kwenda namba 15564, hapo utakuwa umeingia moja kwa moja kama mshindani.