Wachezaji wa Ufaransa wakiwapongeza mashabiki na kujipongeza wao kwa kazi nzuri baada ya kuifunga timu ya Honduras bao 3-0 usiku huu.3-0 ndivyo alivyowahitimishia Ufaransa usiku huu Karim Benzema dhidi ya Honduras.
Karim Benzema akishangilia bao lake la tatu baada ya kuifungia timu yake France usiku huu na hata lile la kwanza na la pili likisababishwa na yeye pia..Pongezi kwake katika mtanange huu ameibeba nchi yake.Kipa wa Honduras N. Valladares alijifunga bao baada ya Karim Benzema kuachia shuti lililogonga posti na kurudi upande wa kipa na kipa kuumalizia mpira huo ndani ya lango lake katika kipindi cha pili dakika ya 48. Dakika ya 72 Karim Benzema amewaongezea tena bao Ufaransa na goli kuwa 3-0 dhidi ya Honduras.Kipa wa Ufaransa akijifunga bao hapa..Unachezea mimi...utajiju!!! 2-0 kwenye neti...Raha ya ushindi ndio hii...Wachezaji wa Ufaransa wakipongezana
France wanapata bao kwa mkwaju wa penati na mchezaji wa Honduras W. Palacios anatolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kumsukuma mchezaji wa Ufaransa Pogba kwenye eneo hatari la kipa.
Karim Benzema anaifungia bao hilo kwa mkwaju wa penati katika dakika za mwishoni mwa kipindi cha kwanza katika dakika ya 45. Ufaransa wanaenda mapumziko wakiwa mbele ya bao 1-0 dhidi ya Honduras.Patashika za hapa na pale zilitokea baada ya mchezaji wa Honduras kumfanyia rafu mbaya PogbaKarim akichonga penati...na kuitangulia mapema Ufaransa bao 1-0......Karim Benzema akishangilia bao alilolifunga kwa mkwaju wa penatiPogba chini Mchezaji wa Honduras Wilson Palacios huku mwamuzi akiwa na yeye!Mchezaji wa Ufaransa Evra chini...chali!!Kikosi cha FranceKikosi cha Honduras
VIKOSI:
France: Lloris, Debuchy, Varane, Sakho, Evra, Pogba, Cabaye, Matuidi, Valbuena, Benzema, Griezmann.
Subs: Ruffier, Cabella, Giroud, Mavuba, Mangala, Sagna, Digne, Sissoko, Remy, Koscielny, Schneiderlin, Landreau.
Honduras: Valladares, Beckeles, Bernardez, Figueroa, Izaguirre, Najar, Wilson Palacios, Garrido, Espinoza, Bengtson, Costly.
Subs: Lopez, Osman Chavez, Montes, Juan Garcia, Jerry Palacios, Mario Martinez, Delgado, Oscar Garcia, Rony Martinez, Claros, Marvin Chavez, Escober.
Referee: Sandro Meira Ricci (Brazil).