Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na mfanyabishara maarufu wa Nigeria Alhaj Aliko Dangote alipokutana naye jijini Abuja, Nigeria, May 8, 2014 pembeni mwa Mkutano wa Dunia wa Uchumi kwa Afrika. Alhaj Dangote ni mwekezaji mashuhuri duniani na hivi sasa anajenga kiwanda kikubwa cha saruji mkoani Mtwara.


Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono baada ya mazungumzo na mfanyabishara maarufu wa Nigeria Alhaj Aliko Dangote alipokutana naye jijini Abuja, Nigeria, May 8, 2014
PICHA NA IKULU