Quantcast
Channel: HABARI NA MATUKIO
Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

NITETEE FOUNDATION YAZINDULIWA RASMI JIJINI MWANZA KUTETEA WANAWAKE NA WATOTO WANAOSHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU TANZANIA

$
0
0
Mama Tizeba (kulia), Mkewa Naibu Waziri wa Uchukuzi ambae alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa taasisi ya Nitetee wakifungua kwa pamoja pazia na Bi Flora Lauwo (kushoto), Mkurugenzi na Muasisi wa Nitetee Foundation kuashiria uzindizu rasmi wa taasisi hiyo katika hafla iliyofajiaka Jumapili ya wiki iliyopita katika Ukumbi wa New Mwanza Hotel, jijini Mwanza.
Mtoto Veronica ambae ni mmoja ya watoto wanaoishi katika mazingira magumu walioibuliwa na taasisi ya Nitetee akitoa ushuhuda wa maisha yake yeye na wadogo zake baada ya baba yao kufungwa jela kwa kesi ya mauaji na kisha mama yao kuwakimbia na kwenda kwa mwanaume mwingine. Kwa mujibu wa Veronica anasema baba yao amefungwa kwa kusingiziwa kwani siku mauaji hayo yakitokea baba yake alikuwa ndani anaumwa, na tukio hilo limezima ndoto zote za maisha yake na wadogo zake.
Meya wa Jiji la Mwanza Mh. Stanislaus Mabula (kushoto) akizungumza na wageni waalikwa (hawapo pichani) na kumpongeza Mkurugenzi wa Nitetee Foundation kwa moyo wake wa kujitoa katika kuwasaidia watu wenye mahitaji maalum. Mh meya aliahidi kufanya kazi na taasisi hiyo katika lengo la kutetea watu wengi Zaidi ambae nae alichangia magodoro sita. Katikati ni Mshehereshaji wa hafla hiyo ambae ni Mtangazaji wa kituo cha Start TV Bi. Ivona Kamontena msanii H-Baba.
Baadhi ya misaada iliyoletwa na wageni waalikwa katika kusaidia familia Zaidi ya 25 zilizokuwa katika mazingira magumu chini ya taasisi ya Nitetee.
Kina mama wajiji la Mwanza walihudhuria hafla ya uzinduzi wa jiji la Nitetee Foundation katika Hoteliya New Mwanza.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>