Quantcast
Channel: HABARI NA MATUKIO
Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

KITU KILICHOSADIKIWA NI BOMU KIMELIPUKA KATIKA BAR YA ARUSHA NIGHT PARK NA KUJERUHI WATU KADHAA JIJINI ARUSHA

$
0
0
Watu kadhaa wamejeruhiwa leo Aprili 13, 2014 na kitu kilichosadikiwa ni bomu la kurushwa kwa mkono lililolipua bar maarufu jijini Arusha ijulikanayo kwa jina la Arusha Night Park (Matako Bar) iliyopo eneo la Mianzini.

Kwa mujibu wa habari ilizozifikia chumba chetu cha habari zinasema kuwa kitu hicho kilichosadikiwa ni bomu kimelipuka kimesababisha uharibifu wa mali ikiwemo kuwajeruhi watu kadhaa.

"Mmoja ya mashuhuda ambaye ameongea na mwandishi wetu kwa njia ya simu amesema tukio hili limetokea saa moja lililopita, ambapo kulikuwa na watu wengi waliokuw wakiangalia mpira.

Mpaka sasa polisi wameshafika eneo la tukio na kuzungushia utepe wa usalama na tayari wameshaanza uchunguzi wa tukio hilo.

KUMBUKUMBU:

June 15, 2013 kulitokea Mlipuko wa bomu katika mkutano wa Chadema.

Mei 2013, bomu lililorushwa liliua watu watatu na kujeruhi wengine zaidi ya 60 katika misa ya uzinduzi wa Kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi Parokia ya Olasiti, mjini Arusha. Misa hiyo ilikuwa ikiongozwa na Balozi wa Vatican nchini na Mwakilishi wa Papa Francis, Askofu Francisco Padila kwa kushirikiana na Askofu Lebulu.

Januari 2, 2014: Wanakwaya sita wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mt. Kalory Rwanga, Usa River, mkoani hapa, wamelazwa katika Hospitali ya Misheni na ya Tengeru, Arumeru baada ya kujeruhiwa kwa bomu. Walikutwa na masahibu hayo juzi muda mfupi baada ya kutoka kanisani kwenye Mkesha wa Mwaka Mpya saa 6.30 usiku, meta 100 kutoka Kanisa hilo, eneo la Kisangani.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

Trending Articles