Katibu Mtendaji wa UNCTAD Dkt Mukhisa Kituyi (Kushoto), Mkurugenzi wa Idara ya Mtangamano wa Biashara wa Wizara ya Viwanda na Biashara Bw Lucas Saronga (Katikati) na Balozi wa Uswizi nchini Olivier Chave(Kulia) wakisaini hati za makubaliano ya utekelezaji mradi wa SECO.
Wafadhili na wawakilishi wa Serikali ya Tanzania walioshiriki uzinduzi wa mradi wa SECO uliofanyika Jijini Arusha.
Washiriki wote wa Mkutano na uzinduzi wa mradi wa SECO uliofanyika mjini Arusha.
Baadhi ya Washiriki wa uzinduzi wa mradi wa SECO uliofanyika Jijini Arusha.
Mradi wa kuunganisha sekta za Wazalishaji matunda, mboga mboga na wenye hoteli (SECO) unaofadhiliwa na Serikali ya Switzerland umezinduli wa Jijini Arusha.
---
Na Mwandishi Wetu, Arusha.
Mradi huo ambao lengo lake kuu ni kuboresha maisha ya watanzania wanaojihusisha na sekta hizo kwa kuongeza uzalishaji wao na uhakika wa masoko ya ndani na nje yanchi, unaanzautekelezaji wake mara moja ukiwa na thamani ya jumla ya Dola za Kimarekani milioni tatu na nusu.
Uzinduzi wa Mradi huo umeshuhudiwa na Katibu Mtendaji wa UNCTAD Dkt Mukhisa Kituyi, Balozi wa Uswizi nchini Tanzania Bw Olivier Chave na Mkurugenzi wa Idara ya Mtangamano wa Biashara katika Wizara ya Viwanda na Biashara Bw Lucas Saronga.