Wiki kama hii, miaka 20 iliyopita, nchi ya Rwanda ilishuhudia kuanza kwa mauaji ambayo kwa siku 99 zilizofuata, yaliacha historia mbaya na ambayo itaendelea kukumbukwa na vizazi vijavyo.
Ndani ya siku 100, watu wanaokadiriwa kufika milioni 1 waliuawa katika mauaji ya kimbari.
Miaka 20 baadaye (mwaka huu), dunia nzima imeungana na Rwanda kukumbuka kile ambacho wengi wanaona kuwa kilitokea na kuachwa kuendelea kutokana na Jumuiya ya kimataifa kutoingilia kati na kutoa msaada muafaka kwa wakati muafaka.
Kumekuwa na matukio mbalimbali kukumbuka mauaji ya kimbari ya Rwanda ambayo yamefanyika duniani kote, Kutoka Kigali Rwanda mpaka hapa Dar-Es Salaam na hata huko Washington DC.
Hii ni sehemu ya ripoti ya Kwanza Production kwenye kipindi cha DAKIKA 90 ZA DUNIA kinachorushwa na kituo cha Radio cha Capital FM cha Dar Es Salaam Tanzania kila Jumamosi kuanzia saa moja na nusu asubuhi (7:30 AM). Hii ilikuwa ripoti ya Aprili 12, 2014