Waziri wa maendeleo ya mifugo na uvuvi dk TITUS MLENGEYA KAMANI leo ametoa pongezi kubwa kwa kampuni ya simu za mkononi ya tigo Tanzania kwa kuanzisha kitengo cha tigo kilimo ambacho kitawasaidia watanzania wengi kutumia mtandao huo kujiendeleza katika maswala ya kilimo ufugaji na uvuvi hapa nchini
Waziri huyo ameyasema hayo leo jijini dare s salaam katika maonyesho ya kilimo yaliyofanyika katika ukumbi wa mlimani city hapa jijini ambapo alipata nafasi ya kutembelea mabanda mbalimbali na kuona shughuli ambazo zinafanywa na wadau mbalimbali wa kilimo
Moja kati ya mabanda Aliyotembelea waziri huyo ni banda la kampuni ya simu za mkononi ya tigo ambalo limekuwa na kitengo maalum cha tigo kilimo yenye lengo la kuwasaidia wafugaji na wakulima nchini.