Mkurugenzi wa Upelelezi wa makosa ya Jinai Zanzibar SACP Yusufu Ilembo, akizungumza na Waandishiwa Habari juu ya kukamatwa kwa majambazi wakiwa na silaha mbili ikiwemo SMG moja na Bastola moja zikiwa na jumla ya risasi 40.
Mkurugenzi wa Upelelezi wa makosa ya Jinai Zanzibar SACP Yusufu Ilembo, akionyesha silaha zilizokamatwa na Makachero wa Jeshi la Polisi Zanzibar kutoka kwa watuhumiwa wa Ujambazi wa kutumia silaha.
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakimsikiliza Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Zanzibar SACP Yusufu Ilembo, wakati akitoa taarifa za kukamatwa kwa watuhumiwa pamoja na silaha.
Silaha na baadhi ya vifaa vilivyokamatwa kutoka kwa watuhumiwa hao wa ujambazi vikiwa mezani mbele ya Waandishi wa Habari.

Baadhi ya Waandishi wa habari wakimsikiliza Mkurugenzi wa Upelelezi wa makosa ya Jinai Zanzibar SACP Yusufu Ilembo, wakati akitoa taarifa za kukamatwa kwa silaha pamoja na Watuhumiwa wa Ujambazi
---
Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi- Zanzibar
Makachero wa Jeshi la Polisi Zanzibar, wamefanikiwa kuzikamata silaha mbili na risasi 40 za Kivita zinazosadikiwa kutumika katika matukio mbalimbali ya kihalifu likiwemo la mauaji ya Askari Polisi mmoja lililotokea Machi 2, mwaka huu huko kwenye Hoteli ya Kitalii ya Pongwe Bay mkoa wa Kusini Unguja Zanzibar.
Katika tukio hilo Askari Polisi mmoja mwenye namba F.5607 Koplo Mohammed Mjombo(44) aliuawa huku mwenzake mwingine mwenye namba F.6198 Konstebo Ibrahim Juma Mohammed(35) akijeruhiwa vibaya kwa risasi kabla ya kuporwa silaha aliyokuwa nayo.
Akizungumza na Waandishi wa Habari ofisini kwake, Mkurugenzi wa Upelelezi Zanzibar SACP Yusufu Ilembo, amesema kuwa pamoja na kukamatwa kwa silaha hizo pia Makachero hao wamewatia nguvuni majambazi watatu kati ya wanne waliohusika katika tukio hilo la mauaji ya Askari Polisi.
Alisema silaha hizo zilikamatwa nyumbani kwa mmoja wa watuhumiwa anayeishi eneo la Mkokotoni katika mkoa wa Kaskazini Unguja zikiwa zimefungwa na vipande vya plastiki na vitambaa na kuviringishwa katika waya mpya wa kupigilia madirisha.
Bila ya kuwataja majina yao kwa sababu za kiupelelezi, DCI Ilembo ameainisha wazi kuwa baadhi ya watuhumiwa hao ni wenyeji wa Pangani mkoani Tanga na wengine ni wenyeji wa Kisiwa cha Pemba Zanzibar.
Amesema katika mahojiano na makachero wa Polisi, Majambazi hayo pia yalikiri kuhusika na matukio mbalimbali katika mikoa ya Viisiwani na Mikoa ya Tanzania Bara matukio ambayo yangali yakichunguzwa katika Vituo mbalimbali vya Polisi.
Watuhumiwa hao pia walipatikana na vitu mbalimbali zikiwemo fedha taslimu shilingi 490,000 za Kitanzania, dolla 75 za Kimarekani, Euro na fedha kadhaa za Kichina pamoja na vitu mbalimbali zikiwemo simu za mkononi.
Amesema bado Jeshi la Polisi linaendelea kuwahoji watuhumiwa hao ili kuweza kuipata silaha ya Polisi aina ya SMG ambayo waliiporwa kutoka kwa Askari wakati walipowavamia na kuwashambuliwa kwa risasi.
Hata hivyo, SACP Ilembo amekiri wazi kuwa kukamatwa kwa silaha hizo pamoja na watuhumiwa, kumetokana na taarifa za siri za Raia wema zilizotolewa Polisi na kupelekea kufanyiwa kazi na kuleta mafanikio hayo.
Amewaomba wananchi katika maeneo mbalimbali kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa za siri zitakazowafichua watuhumiwa wakiwemo waliofanya na wanaotarajia kufanya makosa ili waweze kufuatiliwa na kukamtwa na kufikishwa mahakamani kwa hatua zaidi.