Quantcast
Channel: HABARI NA MATUKIO
Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

MAHAKAMA KUU KANDA YA MOSHI YAAWACHIA HURU WASHTAKIWA 9 NA KUWATIA HATIANI 3 KATIKA KESI YA MAUAJI YA NMB MWANGA

$
0
0
Mshtakiwa namba 3, Kalisti Joseph Kanje (aliyebeba mafaili), Mshtakiwa namba moja, Samwel Gitau Saitoti (alifunika uso) na mwenzake Mshtakiwa namba 2, Michael Kimani wakitoka nje ya mahakama kuu baada ya mahakama hiyo kuwatia hatiani kwa kosa la kuua Askari polisi katika tukio la uporaji wa benki ya NMB Mwanga

Washtakiwa namba 4 hadi 12, wakisaidiwa kupanda kwenye gari la Polisi baada ya mahakama kuu kanda ya Moshi, mkoani Kilimanjaro, kuwaachia huru leo mchana katika kesi ya mauaji ya askari polisi yaliyotokea Julai 11 mwaka 2007.
Mshtakiwa namba 3, Kalisti Joseph Kanje (aliyebeba mafaili), Mshtakiwa namba moja, Samwel Gitau Saitoti (alifunika uso) na mwenzake Mshtakiwa namba 2, Michael Kimani wakitoka nje ya mahakama kuu baada ya mahakama hiyo kuwatia hatiani kwa kosa la kuua Askari polisi katika tukio la uporaji wa benki ya NMB Mwanga.

Mshtakiwa namba 12, Salome Materu aliyekuwa Mhasibu wa Benki ya NMB  Mwanga akisaidiwa kupanda katika gari la polisi baada ya mahakama kuu kanda ya Moshi, mkoani Kilimanjaro, kumuachia huru pamoja na wengine 8 katika kesi ya mauaji ya askari polisi yaliyotokea Julai 11 mwaka 2007.
Mshtakiwa namba 12, Salome Materu aliyekuwa Mhasibu wa Benki ya NMB Mwanga akisaidiwa kupanda katika gari la polisi baada ya mahakama kuu kanda ya Moshi, mkoani Kilimanjaro, kumuachia huru pamoja na wengine 8 katika kesi ya mauaji ya askari polisi yaliyotokea Julai 11 mwaka 2007... (picha zote  na Fadhili Athumani)
Mwandishi Wetu, Kilimanjaro.

MAHAKAMA kuu kanda ya Moshi, imewaachia huru washtakiwa 9 na kuwatia 
hatiani wengine 3 wakiwemo Wakenya wawili na Mtanzania mmoja kwa kosa 
la kumuua askari Polisi E6829 Michael Milanzi, aliyeuawa katika tukio 
la Ujambazi lilitokea Julai 11mwaka 2007 kwenye Benki ya NMB tawi
laMwanga.


Akisoma uamuzi mdogo wa mahakama hiyo, Jaji mfawidhi Kasusulo Sambo alisema kwa mujibu wa sheria wa sheria 293 ya muendelezo wa ushahidi  wa makosa ya jinai, kifungu kidogo cha 1, sura ya 20 kamailivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002, mahakama imeridhia kuwa Jamhuri  ilishindwa kabisa kujenga kesi dhidi ya watuhumiwa 9, Raia wa Tanzania, na hivyo inawaachia huru.

Jaji Sambo alisema katika uamuzi huo Mahakama vilevile ikiongozwa na sheria hiyo kifungu kidogo cha 2, sura ya 20 kama ilivyorekebishwamwaka 2002, imeona kwamba upande wa Jamhuri ilifanikiwa kujenga Kesi dhidi ya mshtakiwa namba 1, Samwel Gitau, Mshtakiwa namba mbili Michael Kimani, wote raia wa Kenya na mshtakiwa namba 3, Kalisti Joseph Kanje, Raia wa Tanzania.

 "Mahakama ilitafakari ushahidi wote wa Jamhuri, na kufikia maamuzi
kwamba mashahidi wote 18 waliofika mbele ya mahakama hii, walionesha
ni jinsi gani Jamhuri ilivyoshindwa kujenga kesi dhidi ya
washtakiwa namba 4,5,6,7,8,9,10,11, na 12,


"Aidha Mahakama hii tukufu imeridhishwa kwamba Jamhuri kwa kuzingatia
sheria ya muendelezo wa makosa ya jinai, kifungu kidogo cha pili, sura
ya 20 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002, ilifanikiwa kujenga
kesi kwa kiwango kisicho mashaka dhidi ya washtakiwa namba 1,2 na
3," alisema Jaji Sambo.



Katika uamuzi huo, Jaji Sambo aliongeza kuwa Mahakama inaamuru
washtakiwa wote 4 hadi 12 walionekana kutokuwa na kesi ya kujibu dhidi
ya tuhuma hiyo ya mauaji waachiwe huru maramoja isipokuwa kama wana
kesi nyingine inayowakabili ambapo mtuhumiwa namba 10, ElizabethMsanze
"Bella" ambaye anatuhuma za ujambazi alilazimika kuendelea
kutumikia kifungo chake.


Washtakiwa walioachiwa huru ni mshtakiwa namba 4, Deodat Temu,
mshtakiwa namba 5, Afande Nathaniel Wanyama, mshtakiwa namba 6,
Emmanuel Mziray, mshtakiwa namba 7, Florian Kimati "Babylon",
mshtakiwa namba 8 Devotha Msanze.


Wengine ni mshtakiwa namba 9, Juliana Msanze, Mshtakiwa namba 10
Elizabeth Msanze, mshtakiwa namba 11, Ntibasalila Msanze na mshtakiwa
namba 12, Salome Materu ambaye alikuwa ni Mhasibu wa Benki hiyo wakati
wa uvamizi.


Wakati huo huo upande wa utetezi unaomtetea mshtakiwa namba 3, Kalisti Joseph, unaowakilishwa na wakili wa kujitegemea, Prof. Jonas Itemba, umetoa ombi la kuwasilisha mashahidi wawili mahakamani hapo kwa ajili ya kutoa ushahidi wa utetezi kwa mteja wake.

Mashahidi hao ni Josephine Kalisti, ambaye ni mke wa Mshtakiwa huyo, 
raia wa Tanzania anayetuhumiwa kushiriki na kufadhili tukio la
ujambazi lililopelekea mauaji, na mwengine ni Dafrosa Joseph.


Kesi hiyo itaendelea kusikilizwa tena Aprili 10 mwaka huu, baada ya
Mahakama kuridhia ombi la Washtakiwa namba 1 na 2 ambao hawana
mashahidi, ya kutaka kuruhusiwa kuwasilisha mahakamani, maelezo ya
Shahidi namba moja aliyoandika kwa mkono wake ambaye ni meneja wa
Benki hiyo wakati huo, Robert Marandu.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>