Wamiliki wa Hoteli za kitalii mjini Bagamoyo wamelalamikia uongozi wa wa Halmashauri ya mji huo, kwakutojali uchangiaji wa mapato yatokanayo na wageni wanaokwenda katika mahoteli kutokana na kuweka kifusi cha mchanga zaidi ya miezi miwili bila kusambazwa hivyo kufanya wageni kushindwa kuenelea na shughuli zao.
Wakiongea kwa wakati tofauti walisema kuwa wanaushangaa uongozi wa halmshauri kususia barabara hizo na kuziacha katika hali isiyoridhisha.