Mke wa Waziri Mkuu Tunu Pinda akimshukuru Mwalimu wa semina ya wanandoa Mchungaji Peter Mitinimgi baada ya kumkabidhi machapisho na dvd za mafundisho ya kudumisha ndoa kulia kwa Tunu Pinda ni Mwenyekiti wa umoja wa akina mama wa new life in chirist mkoa wa Dar es salam Akunda, Nko anayefuatia ni mke wa naibu waziri wa fedha Naima Malima . mama tuni panda alikuwa mgeni rasimi katika semina ya wana ndoa iliyo andaliwa na New life in Christ mkoa wa Dar es Salam. Picha na Chris Mfinanga.
Mama Tunu Pinda akiangalia maonyesho ya majarida yanayo elekeza jinsi ya kudumisha ndoa kulia kwake ni Naima Malima na kushoto kwake ni mwenyekiti wa New life in Christ mkoa wa Dar es Salam, Akunda Nko.
“Wanandoa hamnabudi kujenga maadili mazuri,masikilizano na uvumilivu katika ndoa ili muweze kuepusha uvunjifu wa maadili katika ndoa”. Inaaminiwa kwamba matatizo mengi ya kuporomoka kwa maadili katika ndoa chanzo chake kikubwa ni kukosekana kwa uvumilivu, alifafanua Mama Pinda.
“Ndoa zisipokuwa imara watoto wanakosa malezi, ndoa zinapovunjika, si wanadoa tu wanaoharibikiwa, bali watoto pia hupata majeraha makubwa ya kisaikolojia katika maisha yao,hivyo nawaomba wanandoa kuisha katika imani na masikilizano ili kuweza kudumisha ndoa zenu”, alisisitiza.
Semina hii ni chachu na sehemu muhimu sana ya kujifunza na kukumbushana masuala muhimu ya kujenga ndoa zenu, hivyo mtumie nafasi hii kutafakari hali halisi ya ndoa zenu kwa kuwa wasikivu na wachangiaji wa mawazo na pia kwenda kuwaeleza na wengine kile mlichojifunza: “Naamini semina hii italeta uponyaji na nuru mpya katika ndoa zenu na familia na kuwa kichocheo katika kuimarisha ndoa zenu”, alisema.
Napenda kusisitiza kwamba, hatuwezi kuwa na Taifa la watu wenye maadili mema kama ndoa zenu ambazo ni kiini cha familia, jamii na Taifa hazitaimarishwa, ni dhahiri kwamba hatutaweza kupata viongozi bora ikiwa ndoa zilizo imara ambazo ni kiini cha uhai wa familia zitaachwa ziyumbe:” Viongozi bora hutoka kwenye ndoa bora ni vizuri kujenga utamaduni katika jamii kwa kuwa na ndoa zisizotetereka”alisema Mama Tunu.
Mama Pinda aliwaomba watoa huduma wa "New Life in Christ" pamoja na makanisa na watu wengine wanaotoa huduma za mafundisho ya uimarishaji wa ndoa kufanye jambo hili kuwa endelevu na kuhusisha ndoa nyingi kadri iwezekanavyo. “Serikalini wanasema Matokeo ya Haraka sasa au Big Results Now nami nashauri iwe hivo katika ndoa zenu yawe malengo yenu na yaelekezwe katika kuleta Matokeo Makubwa Zaidi”, aliongezea Mama Tunu Pinda.
Mama Pinda aliwashauri watoa huduma wa "New Life in Christ", kuangalia namna ya kuandaa Semina kwa ajili ya vijana ambao sasa wameingia katika ulimwengu wa utandawazi kwa kuwaaandaa na kuwasaidia waingie kwenye taasisi ya ndoa kwa kumshirikisha Mungu kupata wenza wao kuliko kutafuta wachumba kupitia mitandao ya kijamii kama vile facebook, viber, Instagram na mingineyo. “Semina hizi zitawasaidia kuwajenga kimaadili huku wakitambua majukumu yao kama mume ama mke, kama baba au mama na hatimaye kuishi katika maadili mema”.
Mapema, Mwenyekiti wa "New Life in Christ" Dkt. Alyson Mmanyi alisema huduma kama hizi za semina zinatolewa kwa watu wote wakristo wa madhehebu mbalimbali ili kuweza kunusuru ndoa na uvunjifu wa maadili kwani Taasisi ya ndoa imevamiwa na ndoa bila Mungu haiwezekani.
”Tumekuwa tunatoa huduma za kuhubiri Injili kwa watu mbalimbali ambapo tayari tumeshatoa huduma hizi Mkoani Tarime, Rorya na tunatarajia kwenda Butiama mwaka huu”, alisema Dkt. Alyson.