Mgeni rasmi Mwenyekiti wa Chama Cha Msalaba Mwekundi (Red Cross), Dr. George Nangale, akizindu rasmi kampeni ya ‘Save The Elephant’ (Okoa Tembo) kwa niaba ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete, kama jitihada za kumuunga mkono Rais Kikwete katika kupambana na ujangili wa wanyamapori nchini. Kushoto ni Mratibu wa Taasisi ya Tembo Marathon Tanzania, Bw. Robert Zangi, Wa pili kushoto ni Meneja Uhusiano wa Bodi ya Utalii (TTB), Geofrey Tengeneza, na Kulia ni Dr. Herry Muhando kutoka International Evangelist.(Picha na Zainul Mzige).
Na Mwandishi Wetu
Taasisi ya Tembo Marathon Tanzania imezindua kampeni ya ‘Save The Elephant’ (Okoa Tembo) kama jitihada za kumuunga mkono Rais Jakaya Kikwete katika kupambana na ujangili wa wanyamapori nchini.
Mratibu wa taasisi hiyo, Robert Zangi, amesema wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo kwamba wameamua kumuunga mkono Rais Kikwete kutokana na kukithiri kwa matukio ya ujangili wa wanyamapori miaka ya hivi karibuni.
Aliongeza kwamba kampeni hiyo itawalenga zaidi watu ambao wanaishi jirani na mbuga za wanyama.
“Watu wanaoishi jirani na mbuga za wanyama ni rahisi kufahamu nani ni jangili na nani ni raia mwema miongoni mwao,” alisema.
Aliongeza kusema kwamba kampeni hiyo itawafikia watu wanaoishi jirani na mbuga za wanyama kwa lengo la kuwaelimisha umuhimu wa kupambana na jangili dhidi ya wanyamapori.
Mratibu wa Taasisi ya Tembo Marathon Tanzania, Bw. Robert Zangi, akizungumza na wageni waalikwa wakati wa uzinduzi wa kampeni ya ‘Save The Elephant’ (Okoa Tembo) kupitia Taasisi yake kama jitihada za kumuunga mkono Rais Jakaya Kikwete katika kupambana na ujangili wa wanyamapori nchini. Wa pili kushoto ni Meneja Uhusiano wa Bodi ya Utalii (TTB), Geofrey Tengeneza, Wa pili kulia ni Mgeni rasmi Mwenyekiti wa Chama Cha Msalaba Mwekundi (Red Cross), Dr. George Nangale (kwa niaba ya Rais Kikwete) na Kulia ni Dr. Herry Muhando kutoka International Evangelist.
Kampeni hiyo ina mpango wa miaka mitano ambao kwa kuanzia kutakuwa na matukio matatu makubwa mwaka huu kati ya sasa hivi na mwezi Mei.
Tukio la kwanza, alisema, ni la uzinduzi wa kampeni hiyo na la pili ni kuwasilisha ujumbe wa kampeni kwenye Umoja wa Mataifa nchini Marekani tarehe 9 mwezi Aprili na la tatu litakuwa ni semina juu ya kupambana na mauaji ya Tembo, Vifaru na wanyamapori wengine.
Meneja Biashara wa Qatar Airways Tanzania, Bw. Basel Haydar (kushoto) pamoja na Meneja Mauzo wa Qatar Airways Tanzania, Bw. Emmanuel Okware.
Meneja Uhusiano wa Bodi ya Utalii (TTB), Geofrey Tengeneza akisisitiza jambo ambapo ametoa rai kwa wadau mbalimbali pamoja na mataifa mengine kuunga mkono jitihadi hizi kuhakikisha ujangili unatokomezwa.
Nae Mwenyekiti wa Chama Cha Msalaba Mwekundi (Red Cross), Dr George Nangale, amesema kwamba wanaunga mkono kampeni hiyo kwani mauaji ya wanyamapori ni majanga na kwamba watu wanaoishi jirani ya mbuga za wanyama wanaweza kusaidia sana kwenye mapambano dhidi ya ujangili.
Nangale alikuwa anamwakilisha mgeni rasmi ambaye alikuwa awe Rais Kikwete.
Meneja Uhusiano wa Bodi ya Utalii (TTB), Geofrey Tengeneza, alisema ni vizuri kuendelea kuwalinda Tembo na wanyamapori wengine na kuongeza kwamba kampeni hii ni muhimu sana na akaomba jitihada hizi ziungwe mkono na nchi jirani pamoja na mataifa mengine.
Meneja Biashara wa Qatar Airways Tanzania, Bw. Basel Haydar akizungumzia udhamini wao wa kuwapelekea Marekani wanaharakati wa Kampeni ya "Save The Elephant".
Meneja Biashara wa Qatar Airways Tanzania, Bw. Basel Haydar (kushoto), akikabidhi mfano wa tiketi ya ndege kutoka shirika la ndege ya Qatar watakaosafirisha msafara wa kampeni ya"Save the Elephant" kuelekea nchini Marekani kwa Mratibu wa Taasisi ya Tembo Marathon Tanzania, Bw. Robert Zangi ( wa pili kushoto). Wanaoshuhudia tukio hilo ni Meneja Uhusiano wa Bodi ya Utalii (TTB), Geofrey Tengeneza (wa pili kulia) na Mwenyekiti wa Chama Cha Msalaba Mwekundi (Red Cross), Dr. George Nangale, (kulia).
Meneja Mkuu wa Le Grande Casino, Bw. Costa Cambanis (kushoto) pamoja na timu yake kutoka Le Grande Casino Tanzania.
Afisa Mtendaji Mkuu wa UBL Bank, Bw. Muhammad Tanveer, akizungumzia udhamini wao kwa wanaharakati wa kampeni ya "Save the Elephant" ambao ni kuwalipia ada za uwanja wa ndege kutoka Dar, Doha, Chicago na Denver Colorado.
Afisa Mtendaji Mkuu wa UBL Bank, Bw. Muhammad Tanveer (wa pili kushoto) akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya Dola za Kimarekani 1000 kwa Mratibu wa Taasisi ya Tembo Marathon Tanzania, Bw. Robert Zangi (katikati). Wanaoshuhudia tukio hilo ni mgeni rasmi aliyemwakilisha Rais Kikwete, Mwenyekiti wa Chama Cha Msalaba Mwekundi (Red Cross), Dr George Nangale (kulia), Meneja Uhusiano wa Bodi ya Utalii (TTB), Geofrey Tengeneza (wa pili kulia) na kushoto ni Head of Risk wa UBL Bank, Farooq Hashim Randeri.
Afisa Mtendaji Mkuu wa UBL Bank, Bw. Muhammad Tanveer ( wa pili kushoto) akipongezana na Mratibu wa Taasisi ya Tembo Marathon Tanzania, Bw. Robert Zangi (katikati) pamoja na Meneja Uhusiano wa Bodi ya Utalii (TTB), Geofrey Tengeneza (wa pili kulia).
Meneja Mkuu wa Le Grande Casino, Bw. Costa Cambanis, akizungumza kwenye uzinduzi wa kampeni ya "Save the Elephant" inayoendeshwa na Taasisi ya Tembo Marathon Tanzania ambapo kwa kuunga mkono jitihada hizo za kupamba na ujangili wametoa udhamini wa Malazi kwa timu nzima itakayoenda nchini Marekani.
Meneja Mkuu wa Le Grande Casino, Bw. Costa Cambanis (kushoto) akipeana mkono na Mratibu wa Taasisi ya Tembo Marathon Tanzania, Bw. Robert Zangi (wa pili kushoto) wakati wa hafla hiyo fupi ilyodhaminiwa na hoteli ya DoubleTree by Hilton ya jijini Dar es Salaam.
Afisa Mtendaji Mkuu wa UBL Bank, Bw. Muhammad Tanveer (wa pili kushoto) akiwa pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo.
Pichani juu na chini ni baadhi ya wadau kutoka mashirika ya kimataifa, taasisi za serikali, Frankfurt Zoology Society, WWF pamoja wawakilishi wa balozi mbalimbali nchini waliohudhuria uzinduzi huo.
Wadau wakisalimiana baada ya uzinduzi rasmi wa Kampeni ya "Save The Elephant".